Kikao cha NEC Zanzibar: Karume hataki kuongezewa muda!


Na wewe sasa umeshakuwa yahaya makanisa yalikuwepo zanzibar kabla ya muungano hakuna mauaji wala utabiri wako wa kijinga, ni uchochezi na pengine ni ukereketwa na udini wako (ukristo)

Wanzizabar wanachouliza na wanachotaka ni maelewano katika muungano na in fact ukoloni wa Tanganyika uishe huko, wachague viongozi wao bila dodoma thing ..naona ni sawa..

Waacheni wazanzibar waamue mambo yao, mnajidai mnawapenda sana wa tanganyika walioko zenj kuliko walioko musoma? mbona waliua hao sikuona maandamano? hivi wako wangapi huko zanzibar? wazanzibar wangapi wako bara..serikali gani ya kijinga itafanya hivyo..kweli wewe ni mchochezi na una agenda yako shame..

Huko zanzibar kuna watanganyika, wakenya, burundi, oman, wa norway mara ya mwisho kwenda...wapo hakuna aliyewahi kuwaua wala kuwabagua na wazee wetu wamekuwa wakienda huko miaka nenda rudi wakitokea bara bila shida wala problem

Shida ni ukoloni wenu sasa mnatafute visingizio oh dini ...grow up bana! waacheni wanzibar wakitaka muungano ok! wasipotaka ok! mnang'ang'ania nini? au ndio hizo agenda zenu za kina msekwa, makamba, always wanaopenda muungano ubaki kwa udi na uvumba ni wale wanaotoka ... wameshakununua uzieneze hapa

Wazanzibar only this time you can make "REJESHENI HESHIMA YENU" taifa lenu tutaungana kwa heshima si kwa ukoloni.
 
Mwanakijiji, naungana na wewe, CCJ, ni non issue, Kada Tendwa, amesha take care, ametangaza rasmi, they are busy, sheria inatamka provision registration ni 6 Months. Baada ya hapo ni kusubiri zoezi la kuhakiki ambalo linafanywa na msajili at his pleasure.

Hata kama CCJ watamaliza procedures by March, timu ya Tendwa will be busy na hawatatoa usajili wa kudumu mpaka baada ya deadline. NEC itatangaza ratiba ya uchaguzi soon. Baada ya bunge kuvunjwa Alhamisi Tarehe 5/08/2010.
 
-

- Sio siri kwamba recently Karume amekuwa akijaribu sana kuwa a political genius, lakini kule CC wazee kina Almeir, wako kimya wanamuangalia tu watch siku yake itakapofika!

Respect.

FMEs!
Ni Ali Ameir Mohamed aliyezungumza TBC kwamba, Karume hatavunja katiba, ila akasisitiza katiba inarekebishika.

Kwa maoni yangu, kuna Zanzibar mpya on the making. CCM ZnZ wameamua kukata apron strings za CCM Bara. I doubt kama mahadlines wayahudhuria kikao hiki, wataboycot ila puppets kama kina Khatib will never miss.
 
CCM inawayawaya, mambo yake yako hobehobela, katika ombwe kama hili ndipo palipopasa wanamikakati na wanaharakati wa mabadiliko kupambana kwa nguvu zote ili kuleta mabadiliko, maana CCM inamtafuta mchawi miongoni mwao, mbwembwe zao nyingi zimetuama, wanaweka mambo sawa, sasa hatuwaoni wapiganaji, hatuwaoni makamanda, hatuwaoni wanamageuzi na wanasiasa wenye sera mbadala katika mitaa yetu, wanasubiri huruma , CCM imedoda nao wamedoda.
 

- Siku watakapoajaribu tu, basi Sultan wa Oman ambaye siku zote yuko standby London, atarudi tena mbio sana they cannot afford that wao hutishia nyau tu mpaka wakifika Kamati Kuu ndio hutulizwa, bado Salmin ana nguvu sana na hata siku moja hawezi kukubali kukata mizizi na bara, not yet kwa maoni yangu!

Respect.


FMEs!
 
This time, sio kutishia nyau tena, they have determined backed by political will, dhima ya maridhiano kati ya mwana wa aliyeongoza mapinduzi na mwana wa aliyepinduliwa ambaye ni kibaraka wa nasaba ya sultan.
Tena, mark my words. Salmin is nothing on the new Zanzibar. Baada ya CCM kumfanya ilichomfanya yeye na watu wake, ameshaumwa na nyoka na kamwe hatathubutu kufanya kosa la kurudia makosa. Kitu ambacho I'm trying to establishi now, jee CC hardlines wa ZnZ watakuja CC?. Wasipokuja, its done and over, CCM will loose grip ya Zanzibar forever!.
 
Two difficult situations toka ndani ya nyumba, inahitaji busara na compromise ili kuweka mambo sawa. Swali ni what are the compromises for CCM in these two situations.
 
Two difficult situations toka ndani ya nyumba, inahitaji busara na compromise ili kuweka mambo sawa. Swali ni what are the compromises for CCM in these two situations.
.
Siku zote CCM tmekuwa ikishika mpini mambo ya Zanzibar, na ndio huwa determinant factor, sasa Zanzibar wameamka, na iwapo ni kweli vigogo wa Zanzibar wakikacha kikao, this means, no compromise, no surrender!
 
salute mkuu..
 
Watamukumbuka mzee Kawawa,na hiyo CC wamo akina Chenge,Rostam,Makalla,Makamba ,Lowasa(?),Kingunge(?),Msekwa sijui kweli kama kutakuwa na Hekima na Busara za kutoa maamuzi kwa hiyo first eleven ya CCM naona kutakuwa na maamuzi ya mizaha,vitimbi,mipasho na kutishana lakini kama alivyoaandika MMJ mambo ya Zenj ndio issue hasa na Wa zenj yakhe yanapokuja mambo yao hawasikia la shekhe wala muadhini,nikiangalia huo moto mzee Ben angeweza kuuzima lakini kwa sasa tumwache mzee wa watu apumzike kama alivyonukuliwa JK na pia nahisi Ben kaona ajikalie kimya baada ya JK kumvua nguo hadharani
 

Kichuguu, Karume si ametamka hadharani kuwa hatogombea tena? na alitumia ile Jan 12 kuwaaga rasmi wa Zanzibar, sasa vipi tena?
 
Inaonekana watu wengi bado hatujaielewa nguvu ambayo Zanzibar inakuja nayo safari hii
 
Sina mengi
mungu asikilize kilio cha wana jf ccm igawanyike
watenda haki wazidi kuwa na haki;wachafu waendelee na uchafu wao
tosha
 
Inaonekana watu wengi bado hatujaielewa nguvu ambayo Zanzibar inakuja nayo safari hii
.
Hii ndio maana halisi ya JF, kile ulichoelewa, unakileta hapa na kuwaelewesha na wengine, hina unachoelewa kitapitishwa kwenye mizani ya uelewa wa wengine kwa kuungwa mkono/critic na ni katka mchakato huu, wakuelimika huelimika.
Idumu JF.
 
Tunaona chama kipya cha siasa, CCM mpya, Zenji mpya........

Woga wa watawala kutokea hayo ya juu ni nini?
 
Historia inatuonyesha wazi viongozi wa Zanzibar muda unapokwisha wa kukaa madarakani hawapendi kuondoka.Salmin alijaribu kubadili katiba ili aedelee kukaa madarakani kwa kisingizio yeye pekee ndio mwenye uwezo wa kuishinda CUF.Dr Aman nae anamtumia Maalim kuongeza muda na kuna kila dalili safari hii mambo yanweza kuwa mabaya kwa upande wa CCM ikiwa hawatayapa uzito unaostahili.

Kuna hisia CCM bara hawapendi kuona maradhiano baina ya CUF na CCM Zanzibar,nadhani kuna maslahi ambayo mpaka sasa nashindwa kubaini kwanini Tanzania bara tunalazimisha muungano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…