JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imetumia muda wa saa mbili kumaliza kupitia upya shauri la mchezaji Feisal Salum ‘Fei Toto’ na Klabu ya Yanga linalohusiana na mkataba baina ya pande hizo mbili.
Shauri hilo lilianza kusikilizwa saa 5:20 asubuhi na kumalizika saa 7:20 mchana ambapo pande zote mbili ziliondoka eneo la tukio, katika ofisi za TFF Karume Dar es Salaam.
Hayo yalikuwa mapitio ya pili baada ya mwanzo TFF kuamuru kuwa Fei Toto ni mchezaji halali wa Yanga na anapaswa kurejea kikosini lakini upande wa mchezaji huyo haukukubaliana na majibu hayo na kuomba mapitio ‘Review’.
Wakili Fatuma Karume maarufu kama 'Shangazi' aliyekuwa upande wa Fei Toto amesema: "Tumemaliza tulichokuwa tunakifanya, tumewaachia wao watafakri upya, mimi nina mwakilisha tu (Fei Toto), kijana ana haki ya kuamua yeye kama anataka kurudi au vinginevyo, tunasubiri maamuzi. Feisal namjua, kuja kuniomba mimi kumsaidia si kitu kibaya."