"UPINZANI WA KWELI KATIKA NCHI HII UTATOKANA NA CCM. CCM WAKIVURUGANA WAKATENGANA, HAPATAKUWA NA CHAMA TAWALA TENA, HIVYO ITAKUWA RAHISI KWA MTU YEYOTE ATAKAYEKUBALIKA KUINGIA MAHALI PATAKATIFU, IKULU" Kwa miaka mingi CCM imeliongoza Taifa hili kwa kujiamini na kuchukulia kila kitu ni rahisi. Na cha ajabu zaidi kila aliyekuwa tofauti na msimamo wa chama Bungeni kwa awamu moja, kipindi kilichofuata aliondolewa mapema kwenye kura za maoni. Naomba tuamini kuwa kipindi hicho kimepita. Kwa sababu ya kulindana na kushikilia msimamo wa chama pasipo kuelewa hata shabaha na maslahi ya yule aliyeuleta, nchi yetu imejikuta ikingia mikataba mfu inayoididimiza kila kukicha. CCM kama imechoka madaraka ifanye lile linalotamaniwa na watu wengi; "IWAZIBE MIDOMO WALOPOKAJI" Sipendi kuamini kama wanaharakati wa kweli wanaochomoza ndani ya CCM wakifanyiwa kinyume watapata ujasili wa kusubiri hisani ndani ya chama, na ninashawishika kusema wanakubalika kwa wananchi hata wasipokuwa na chama (kama serikali itashindwa tena kesi). Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Tubariki Wavuja Jasho.