Kikawaida MCHAKATO ni jambo lisilokwepeka katika asili ya ulimwengu

Thecoder

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2015
Posts
2,620
Reaction score
6,780
Bila shaka mko vizuri wakuu…

Niliwahi kusema ya kwamba dunia ni sehemu ambayo inautaratibu wake na kutokana na asili hiyo basi maeneo mengi ya kitaasisi au ya kimifumo yameweza kulazimishwa, na yenyewe ili yaweze kwenda sawa lazima utaratibu fulani uwekwe na hakuna jambo lolote linaloweza kufanywa nje ya utaratibu huo.

Kwahiyo katika namna hiyo hiyo pia ni ngumu sana kufanya jambo lolote la kidunia pasipo kufuata utaratibu wa asili ya ulimwengu wenyewe na likadumu kwenye mifumo yake ipasavyo.

Sasa, kikawaida huwa kuna taratibu kadha wa kadha ila moja kati ya taratibu nyingi ambazo zipo katika mfumo wa asili ya ulimwengu ni MCHAKATO.

MCHAKATO ni jambo la kiutaratibu wa asili ambao ndani yake limebeba matokeo ya jambo lolote ambalo linataka au linatakiwa lisimikwe kwenye uso wa dunia au ulimwengu kwa ujumla.

Na ndani ya MCHAKATO huwa kuna hatua kuu mbili muhimu, ambazo ni nguvu za asili za uumbaji wa ulimwengu pamoja na muda wa kiMungu(hii naomba uiweke akilini kwa maana ndio imebeba hii mada).

Muda huwa ni hatua inayotokea yenyewe pasipo mtu ambae anataka jambo lake liweze kusimikwa kuulazimisha, na muda huwa uko locked na ili uwe unlocked ni lazima hatua ya kwanza ya MCHAKATO ifuatwe kiufasa na kinyume chake huwa muda huo wa kiMungu hauwezi kutokea.

Na katika hatua hizo mbili, hiyo hatua ya kwanza ambayo ni ya nguvu, huwa ni jukumu lako wewe na muda huwa ni jukumu la kiMungu (wacha twende taratibu hapa ili tuelewane vizuri).

Ni hivi, nguvu kuu za asili za uumbaji au usimikaji wa jambo lolote katika uso wa dunia au ulimwengu kwa ujumla ni zile zile ambazo niliwahi kuziandika kwenye ule Uzi ambao nilipost kwenye lile jukwaa la biashara, ambazo ni wazo au maono, usaidizi, maarifa pamoja na uwezo wa kufanya kazi.

Na nilisema ya kwamba wakati wa hatua ya kwanza ya mchakato wa Kila jambo lenye nia ya kudumu au kubaki kwa muda mrefu kwenye uso wa hii dunia huwa linapita kwenye Kila nguvu iliyopo kwenye hizo nguvu nne.

Na endapo jambo lolote litashindwa kupitishwa kwenye nguvu hizo nne huwa linashindwa kuunlock au kufungua kile kipengele cha muda kilichopo kwenye hatua ya pili ya MCHAKATO.

Kwahiyo kama ni biashara umeianzisha na unataka ikupe matokeo chanya na iweze kukua na kufikia kwenye ile hatua ya kampuni au jambo kubwa zaidi ya hapo utajikuta unastruggle kufikia hiyo hatua na badala yake utakua unalazimika kurudi nyuma kwenye msingi wa hiyo biashara mara kwa mara ila bado hutaweza kwenda mbele zaidi ya hapo kwa maana muda bado haujawa unlocked kutokana na kosa la kuruka hatua ambalo umelifanya.

Na katika hizi nguvu wazo au maono huwa ndio nguvu ya kwanza inayomjilia mtu ndani yake na mara nyingi wazo au maono huwa ni jambo la kiMungu ambalo huja kwa njia ya hisia au matamanio ya kimsukumo wa kiroho wa kutaka kufanya jambo fulani lenye athari chanya kwenye ulimwengu.

Kila jambo lenye athari chanya katika ulimwengu huwa linasaidia kuongeza mitetemo na kuendelea kuifanya dunia iwe sehemu salama ya kuishi.

Na jambo lenye mlengo huu ambalo humjia mtu kwa msukumo mkubwa sana ambao haukupata kutokea kwa mambo mengineyo aliyowahi kuyafanya, basi jambo hili huwa ni la kihatima.

Kwahiyo maono au mawazo yanayomjilia mtu kwa msukumo mkubwa mara nyingi huwa yanabeba hatima ya mtu huyo

Na pindi unapoamua kuyafanyia kazi hayo maono basi hapo unakua umeamua kupiga hatua kuelekea kwenye hatima yako (hapa naomba usisahau pia ya kwamba Kila kwenye chanya huwa kuna hasi iliyo pembeni yake).

Lakini sasa, hapa kwenye hatima huwa kuna hatima za kiasili ya uumbaji, hizi huwa ni kama mchango wa Kila mtu kwenye huu ulimwengu na wala hazina athari ya moja kwa moja ya kimwili ila zinaweza zikabadili kwa kiasi fulani mtindo wa maisha yako ya kimwili ki namna fulani.

Na hatima za namna hii huwa nguvu na muda huchanganyana kwa maana zikifanyika na kufikia kwenye hatua fulani basi muda huwa unakua unlocked na unachukua nafasi kabla ya hizo nguvu zote nne hazijatumika na baada ya muda fulani basi zile nguvu ambazo hazikutumika hapo awali lazima zitumike ili jambo liweze kusimikwa kwenye ulimwengu na kinyume chake huwa haliwezi kutokea kwa maana mchakato utakua umefeli.

Kwahiyo hatima hizi ukionesha tu kuwa interested nazo basi universe inakua involved kwa haraka sana kwa maana zinaihusu yenyewe moja kwa moja na wewe baada ya kutimiza hatua fulani ya zile nguvu kuu nne, muda unakua unlocked kisha utasubiri hadi pale alam itakapo lia ya kwamba sasa ni muda wa kumalizia zile nguvu ambazo zimebaki za kwenye hatua ya kwanza ili tuweze kukamilisha huu mchakato na wewe utafanya hivyo then jambo linatokea.

Mfano wa haraka haraka ni mchakato wa kutafuta mtoto, huwa wazo linapomjia mtu mume na kuamua kutafuta msaidizi ili awe mbeba maono yake ambae ni mtu mke na endapo huyo mtu mke atakubaliana na wazo la mtu mume basi watashiriki tendo na baada ya tendo muda unakua unlocked na hapa wao wanakua hawana cha kufanya zaidi ya kulazimishwa kusubiri hadi alam itakapolia ya kuwaambia nini cha kufanya.

Ukiuchambua huo mchakato utaona ni nguvu za aina tatu huwa zinatumika kabla ya muda haujawa unlocked na kama itatokea nguvu ya aina moja itakosekana kati ya hizo tatu basi muda utashindwa kuwa unlocked na badala yake mtalazimika kurudi kwenye msingi wa mchakato upya(na hii ni kwenye Kila jambo ambalo hutaka kusimikwa duniani).

Sasa kwenye huo mfano ni kwamba, nguvu ya kwanza ni wazo ambalo limemjia mtu, na nguvu ya pili ni ile ya usaidizi kwa maana yule ambae alipokea hilo wazo na kukubali kuwa mbeba maono, na nguvu ya tatu ni ya maarifa ambayo hii hutumika kwenye kujua namna gani wafanye ili kuweza kuyatafsiri hayo mawazo au maono yaweze kuwa kwenye namna ya kilimwengu, na hapa ndio maarifa ya kujua namna ya kuusoma ule mzunguko wa mwanamke ili kujua tarehe ambazo mimba inaweza kutungwa lakini pia kujua mke na mume wanatakiwa kufanya nini ili hiyo mimba iweze kutokea(mfano kuweka viungo kwenye maeneo husika na mwanaume kuhakikisha mbegu zinatoka).

Na baada ya hizo nguvu tatu kufuatwa kwa ufasaha basi muda unakua unlocked na baada ya hapo wahusika wanakua hawana cha kufanya na badala yake wao wanaiachia asili iweze kufanya kazi yake na hapa huwa ni asili ya kiroho na wala si kimwili.

Kwahiyo baada ya muda kumaliza kazi yake basi alam italia na nguvu ya mwisho ambayo ni ile ya uwezo wa kufanya kazi bila kujali ugumu wa kazi yenyewe itaenda kuwa applicable na hapa ndio mama sasa atatakiwa aiapply hii nguvu ili kuhakikisha mchakato unakamilika na akishindwa basi mambo huaribika na hiyo project itakua imeishia njiani.

Sasa huu ni mfano wa haraka ambao Mimi nimekupa ila kuna mifano mingi ambayo ipo katika nyanja mbalimbali za maisha na inafuata huu utaratibu na ile ambayo imeshindwa kufuata mchakato kwa ufasaha haikuweza kuonekana kwenye uso wa dunia kwa maana ilikufa.

Okay, najua unandoto kubwa za kufanikiwa ila kuna mahala umekwama na unashindwa kwenda mbele zaidi ya hapo, basi ni vyema uweze kurudi nyuma kwanza uweze kuangalia ni hatua gani ya kimchakato haiko applicable kwenye hiyo project yako kiasi cha kufanya muda ushindwe kuwa unlocked.

Hatuwezi kuvuna bila kupanda, na hadi kufikia hatua ya kupanda ni MCHAKATO umefanyika na nguvu zimekua applicable.

Nguvu ya kwanza ni wazo au maono ambayo humjia mtu ya kwamba sasa nataka kulima, na nguvu hii haiwezi kutimia kama haitakua na mtu ambae atatia nguvu ya usaidizi, huyu ni mtu ambae ataisimamia hiyo nguvu ya maono hadi kwenda kuwa halisi.

Nguvu ya usaidizi huwa haiwezi kufanya kazi kama wazo halijatafsiriwa na kuwa katika namna ya kidunia kwa maana lazima nguvu ya maarifa iweze kuingia hapo, baada ya wazo kutafsiriwa na kuwa kwenye mfumo wa kidunia lazima nguvu ya kufanya kazi pasipo kujali ugumu wa kazi yenyewe iweze kuingia kati na baada ya hapo basi muda utakua unlocked na mwenye wazo atatulia hadi pale muda utakapoleta alam ya eidha kuna nguvu inahitajika iongezwe tena kati ya zile nne au laa.

Katika mfano huo tukiuchambua ni kwamba, kabla mtu hajalima lazima wazo limjie kichwani mwake ya kwamba mwaka huu nataka kulima zao fulani, na mtu anaejiliwa na hili wazo anaweza asijue zao hilo anatakiwa alilime wapi na kwenye ardhi yenye sifa zipi hilo zao linastawi zaidi na hatua gani anatakiwa azifuate ili zao lake liweze kustawi kwa uzuri lakini pia budget kiasi gani yaweza kutosha kwenye kukamilisha huo mradi wake.

Ili aweze kujua hayo yote lazima amtafute mtu mwenye nguvu ya maarifa aweze kumtafsiria hivyo vyote pamoja na kumpatia takwimu sahihi za miezi ya kulima na kadhalika.

Baada ya mtu wa kutafsiri kumaliza kazi yake basi lazima itaitajika nguvu ya usaidizi ili iweze kuelekea eneo la tukio kwenda kusimamia huo mradi wenyenyewe na kuiweka ile tafsiri kwenye vitendo.

Nguvu ya usaidizi haiwezi kufanya kazi pasipo kuwepo na nguvu ya uwezo wa kufanya kazi pasipo kujali ugumu wa kazi yenyewe, kwahiyo hiyo lazima iingie ili shamba liweze kusafishwa, na watu waweze kulima na kuweka udongo kwenye yale mazingira yanayotakiwa kwa kuzingatia ile tafsiri ya mtu mwenye ile nguvu ya maarifa na baada ya hapo mbegu ziweze kupandwa .

Na baada ya hatua hizo nne kukamilika basi hatua ya pili ya MCHAKATO ambayo ni muda inakua unlocked hapo hapo na kuwafanya watu waendelee kusubiri asili iweze kufanya kazi yake huku wakiwa makini kuskiliza alam ambayo muda utakua unatoa kwenye Kila hatua hadi pale kipindi cha mavuno kitakapo wadia na hivi ndivyo mambo yote yanavyosimikwa katika uso wa dunia, MCHAKATO ndio asili ya ulimwengu juu ya mambo yenye kuhitaji usimikwaji.

Najua pengine hii nayo ni asili ambayo inashangaza ila ndio hivyo hakuna mafanikio pasipo MCHAKATO wenye kufuata hatua hizo mbili.

Na kwenye hizo hatua zote mbili, muda ndio ambao umebeba kweli ya unachotaka kukisimika, ikiwa kinafungamana na wewe basi muda utakuambia na ikiwa havifungamani na wewe pia muda hautaacha kukuambia.

Ikiwa kuna nguvu haikuwekwa ipasavyo kutoka kwenye ile hatua ya kwanza ya MCHAKATO basi muda utakuambia na kama nguvu zote ziliweza kuwekwa ipasavyo pia muda hautaacha kukuambia.

Lakini nataka ujue ya kwamba kwenye kila jambo ni rahisi kujua ya kwamba sasa ni wakati wa kuupa muda nafasi kwa maana hii ni hatua ambayo lazima ije pindi tu mtu anapokua amemaliza zile hatua za awali za MCHAKATO.

Ila si Kila jambo linaweza kukupa alam ya moja kwa moja ya kwamba sasa muda umeshamaliza kazi yake na sasa tayari jambo lako limeshasimikwa kwenye hii dunia au laa.

Ila badala yake huwa tunaangalia pale ambapo tutaona jambo limeanza kuleta ile athari chanya ambayo ilikua inatarajiwa ililete kwenye jamii husika.

Na ni kwa muda gani sasa mtu anatakiwa aupe muda nafasi? Ni hadi pale utakapoona umeweka nguvu zote kwa usahihi na kwa muda mrefu umekua ukiendelea kupush jambo lako lakini hauoni matokeo yale ambayo uliyatarajia.

NITARUDI…
 
 
Mtu atajuaje au atapata ishara gani kwamba muda umefika
Kiuhalisia hakuna mtu anaejua tarehe yake ya kufanikiwa ila Kila mtu anajua tarehe ambayo ataanza kufanya jambo fulani ambalo anatarajia liweze kumpa mafanikio ya kifedha hapo mbeleni.

Hakuna mtu anaejua tarehe rasmi ya ujenzi wa nyuma yake utakayo kamilika zaidi ya ahadi kutoka kwa mafundi ambazo mara nyingi huwa ni kama probability kwa maana lolote linaweza kutokea ila Kila mtu huwa anajua tarehe ambayo atamuita fundi aje achimbe msingi wa kuanza kujenga hiyo nyumba.

Kila mkulima anajua tarehe ya kupanda mbegu shambani mwake ila hajui tarehe ambayo atakuja kuvuna.

Haya yote ni mambo ya kimchakato ambayo ndani yake kuna hatua ambayo ni ya wewe na kuna hatua ambayo si yako na ndio maana ni ngumu kujua muda unaenda kuishia wapi isipokua zingatia hizo indicator ambazo nimezitoa mwishoni mwa andiko langu mama hapo juu.
 
Haupati madhara ila kuna sehemu utakwama kwa maana mzani utakua bado haujabalansi kiasi cha kuunlock hatua ya pili ya MCHAKATO iweze kuchukua nafasi
Mfano; Napika ugali. Badala ya kukoroga uji kwanzia mwanzo. Me nikasubiri maji peke yake yachemke kisha nikasonga ugali. Hapo unakua ugali au sio ugali? Na unaweza kuitofautisha ikiwa utaletewa mezani bila kuambiwa imepikwa kwa mchakato gani?
 
Binafsi naamini, vipo unavyoweza kuruka hatua fulani na ukapata matokeo yale yale sawa na mtu aliefuata hatua zote zilizozoeleka. Na vipo ambavyo havifai kuruka hatua hata moja ili kupata matokeo. Kikubwa ni kujweza kuvitofautisha katika utekelezaji wako.
 
Mfano; Napika ugali. Badala ya kukoroga uji kwanzia mwanzo. Me nikasubiri maji peke yake yachemke kisha nikasonga ugali. Hapo unakua ugali au sio ugali? Na unaweza kuitofautisha ikiwa utaletewa mezani bila kuambiwa imepikwa kwa mchakato gani?
Hata usipokoroga uji lazima utafuata hatua za kimchakato, wazo linakujia la kupika ugali, unatafuta namna ya kubadili hilo wazo kuwa kwenye uhalisia na hapo ndipo maarifa ya moto, unga, maji, na makadirio yake yanapochukua nafasi, na unatafuta kitu cha kukusaidia ili ugali uweze kutokea ambapo hapo itakua mwiko, banio la kukusaidia kushika na kadhalika na bila nguvu za kusonga huo ugali hauwezi kutokea ugali na baada ya kusonga basi utasubiri muda uchukue nafasi yake ili ugali uive na muda ukimaliza nafasi yake basi kaharufu kazuri kakukujulisha kwamba ugali wako uko tayari kwahiyo unaweza kuutoa ili ukaendelee kuukula😅😅
 
Hauwezi labda kuwe na mchakato invisible au uwe ulishafanyika na watu wengine then wewe unakuja kumalizia, ila vinginevyo ni ngumu sana.
 
  • Je, ni kwa namna gani mtu anaweza kutambua kuwa yuko katika hatua sahihi ya mchakato wa kusimika jambo lake?
  • Ni vigezo gani vinaweza kumsaidia mtu kutambua kuwa amekosea hatua fulani katika mchakato wake wa mafanikio?
 
Naomba nisaidie hapa.
  1. Katika mfano wa uzazi, umetaja kuwa hatua tatu za kwanza lazima zifuatwe kabla ya muda kufunguka. Je, kuna matukio ambayo asili inaweza kuingilia kati hata kama baadhi ya hatua hizo hazikufuatwa ipasavyo?
  2. Katika mfano wa kilimo, umesema kuwa baada ya kupanda mbegu, muda unakuwa unlocked na kazi ya binadamu inakuwa ndogo. Lakini vipi kuhusu hali kama ukame au wadudu waharibifu—hizi zinahusianaje na dhana ya muda wa KiMungu?
 
Huyu mkuu, Thecoder, ana madini adhimu sana, mfano mwingine unakua masikini unapata wazo la kwenda kwa mganga kinachofuata ni kujua huyo mganga utampata wapi unauliza wajuvi wanakuelekeza unafika kwa mganga anakupa madawa na masharti then unatekeleza maagizo yote halafu bwana muda anachukua nafasi yake siku saba zinakamilika alarm inalia utajiri unapiga hodi, hahaaaaaa.
 
  • Je, ni kwa namna gani mtu anaweza kutambua kuwa yuko katika hatua sahihi ya mchakato wa kusimika jambo lake?
  • Ni vigezo gani vinaweza kumsaidia mtu kutambua kuwa amekosea hatua fulani katika mchakato wake wa mafanikio?
Kujua kama upo kwenye hatua sahihi ni pale ambapo wazo lako tayari limetoka kwenye hatua ya wazo la kichwani hadi kuwa kwenye hali ya kidunia ambayo haihitaji tena hadithi kwa watu bali ni Kila mtu anaona.

Muda ndio ambao utakupa taarifa ya kwamba kuna hatua haiko sawa kwahiyo inatakiwa kuwekwa sawa ili scanning iendelee.

Chukulia mfano huu ya kwamba tuseme umejiwa na wazo la kuanzisha product yako ya kushikika, labda tuchukulie ni sabuni.

Utaweka size nguvu kuu nne zilizo kwenye asili ya uumbaji ili kuhakikisha ile hatua ya kwanza inakamilika, na utapata kufahamu ya kwamba hatua ya kwanza imekamilika pindi ambapo sabauni zinakua mkononi mwako tayari kwaajiri ya matumizi.

Ikiwa sabuni hii ilitengenezwa maalumu kwaajiri ya kutibu tatizo fulani la ngozi na ikatokea wakati wa kutumia hilo tatizo likawa halitatuliwi basi hapa utajua ya kwamba kwenye zile nguvu nne kuna nguvu ya maarifa haikuwekwa kwa kiwango kinachotakiwa.

Na kama ikitokea wazo lako baada ya kumtafuta mtu mwenye nguvu ya maarifa na kuanza kuongea nae ili aweze kulitafsiri hilo wazo lako liwe kwenye mifumo ya kidunia na ikatokea akakuambia unachokiwaza hakiwezekani kuwa kwenye uhalisia kwasababu moja mbili tatu, basi utajua nguvu ya maono au mawazo yako haikua kwenye kile kiwango chenye kufaa.

Ikitokea sabuni zako zikawa zimefanikiwa ila zikawa zipo kwenye package ambazo wewe hukuzitegemea au katika maumbo ambayo hayavutii hapa utajua nguvu ya usaidizi ilipungua na kama ulitarajia awamu ya kwanza utoe sabuni elfu kumi then zikatoka sabuni elfu saba basi utajua nguvu ya utendaji kazi ilipungua.

Na hivyo ndivyo mambo yatakavyokwenda kwenye Kila jambo.
 
Yeah ukishaweka hizo nguvu zote huwa muda lazima uingilie kati na kwenye muda hapo ndipo ambapo udhaifu wa nguvu fulani utaenda kuonekana kwa maana muda utakuletea alam ya kwamba ni kweli uliweka nguvu zote lakini kuna nguvu hii kwenye hatua ya awali ya MCHAKATO haiko kwa kiwango kinachotakiwa so na wewe utaendelea kuongeza kwa Kila alam inavyolia.

Ukame ni jambo la muda ambalo na lenyewe likitokea lazima alam italia ya kwamba hapa sasa kuna ukame kwahiyo kama kuna mto jirani itabidi urudie mchakato wa kutoka kwenye hatua ya kwanza ambao ni mchakato wa nguvu ya maarifa pamoja na ile nguvu ya kufanya kazi kwa nguvu na hata ile ya usaidizi na kuhusu wadudu pia ni swala la muda na likitokea muda unakupa alam ya kwamba kuna wadudu kwahiyo inabidi nguvu ya maarifa iongezwe na ile ya kufanya kazi bila kuchoka kwa maana nguvu ya maarifa kujua ni dawa gani itafaa kuua hao wadudu na nguvu ya kufanya kazi ni kwaajiri ya kuanza kupulizia hiyo dawa.

Na nguvu zinazotakiwa huwa ni nne ila kuna baadhi ya mambo yenye kufungamana moja kwa moja na ulimwengu once ukiyaanza tu basi ulimwengu unakua involved na ukiweka nguvu kadhaa basi muda unakua unlocked ila si kwenye mambo yote huwa iko hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…