Mimi siupendi uongozi wa Mangungu hata kidogo, cmpendi pia Try Again wala Ceo Iman Kajula.
In a nutshell, wameshindwa kuleta furaha Simba na hawastahili kuendelea kutuongoza kabisa kabisa.
Lakini hata kama siwapendi je ni sahihi kuhamasisha ama kuchochea mashabiki kwamba mpira ukiisha tuwasake uwanjani na kuwashughulikia?
Je kama Mangungu angedhurika au Try again au Iman Kajula kwa maneno ya GB64 nani angewajibika?
Mnaomtetea GB64 hamuoni kuwa ametenda kosa la jinai?
Kufanya uchochezi hamjui ni kosa la jinai?
Je mashabiki na wanachama hamjui njia sahihi za kuuondoa uongozi?
Zipo njia nyingi za kuukataa uongozi wa Mangungu, try again na bodi nzima lakini sio njia hii ya kudhalilisha viongozi.
GB64 ni nani? Ni mtoto wa juzi tu ametafuta kiki amelala mahabusu, mbona sisi simba lia lia tumeona uongozi haupo serious tumekaa kimya tunatafuta njia nyingine ya halali kabisa kuuondoa uongozi, sio mapinduzi wala nn, hekima na busara zitatumika kuwashurutisha waachie timu.
Mnaompenda GB64 nendeni mkakiri kosa kwa uongozi wa simba ili mambo yaishe na sio kupiga kelele bila hoja za msingi, suala la GB64 ni la kisheria na kiutawala, mkilalamika kwenye mitandao ya kijamii haiwasaidii.
Tujifunze kukosoa viongozi wetu kwa staha na adabu.