Kikokotoo cha retirement ni utekelezaji wa ilani ya CCM

Kikokotoo cha retirement ni utekelezaji wa ilani ya CCM

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,252
Reaction score
36,513
Maamuzi yanayopitishwa na Baraza la Mawaziri ili kuwa sheria ni muswada unaopitia michakato mingi ndani ya serikali.

Rais ambaye ndiye mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri ndiye Mwenyekiti wa Taifa wa CCM ambapo kupitia wasaidizi wake ndani ya chama na serikalini wanaangalia uwiano wa maamuzi ya kisiasa yaendane na ilani inayoongoza serikali.

Slogan ya CCM kwamba ni chama cha wakulima na wafanyakazi ni slogani mufilisi kwa sababu inatumiwa na wafanyabiashara ambao wameingia madarakani na wanawekana kwenye kila nafasi ya maamuzi ndani ya chama na serikali.

Hivyo inawezekana kipengele cha kikokotoo kisionekane kwa macho dhahiri ndani ya ilani ya CCM lakini uwepo wa sheria iliyopitishwa haiathiri uwepo ama utekelezaji wa ilani ya chama.

Hivyo wafanyakazi wa Tanzania tambueni kwamba kikokotoo cha mafao ya kustaafu ambapo michango yote ya mfanyakazi na ya mwajiri ni mali ya serikali hivyo hata uwekezaji unaofanywa na mashirika ya hifadhi ya jamii ni uwekezaji wenye tija kwa wafanyabiashara yaani viongozi wa CCM waliomo serikalini na ndani ya chama.

CCM siyo chama kinachosimamia maslahi ya wafanyakazi na wakulima bali ni chama kinachosimamia na kulinda maslahi ya wafanyabiashara ambao ni viongozi wa serikali na ndani ya chama.

2025 haipo mbali. Lakini niwaase. Msiache kumuomba Mungu wa Mbinguni awape ujasiri wa kuwapa kura viongozi wenye nia ya kushughulikia matatizo ya nchi na wananchi.
 
Inapokuja kwenye kura tunajali mno ujinga wetu na unyonge wetu kuliko kitu chochote.Tuache tu na akili hizi za kupewa kofia
 
Inapokuja kwenye kura tunajali mno ujinga wetu na unyonge wetu kuliko kitu chochote.Tuache tu na akili hizi za kupewa kofia
Tunaambiwa kuwa wapinzani wataleta vita lakini kumbe kauli za vinara wa CCM zinazizima kwenye majukwaa kwamba hata kura ziamue. Katu hawatolubali kuachia madaraka kwa mshindi.

Vita ni sehemu ya ilani ya CCM ndo maana wanajiaminisha wanazo silaha za kumalizana na yeyote ambaye no tishio kwao ktk kunyakua madaraka
 
Nampongeza Magufuli kwa kukianzisha kikokotoo hiki hakika kimeboreshwa sana na pia niipongeze ccm kuwa kikokotoo kipo kwenye ilani yake
 
Kikokotoo kipya ni kaburi la wastaafu, wagonga meza Mungu anawaona...
 
Back
Top Bottom