Kikokotoo kipya cha mafao ya wastaafu chaanza kutumika rasmi

Kikokotoo kipya cha mafao ya wastaafu chaanza kutumika rasmi

Chui mnyama

Member
Joined
Apr 2, 2017
Posts
67
Reaction score
33
Habari wana JamiiForums wenzangu

Kwa wale mliofunga mfungo wa mwezi mtukufu salaam alaikum
Leo nimekuja mbele yenu tujadili Kidogo mambo makuu mawili jambo la kwanza ni juu ya kikokotoo cha pension cha wastaafu na matumizi ya kikokotoo kipya.

Ndugu wanaJamiiForums najua katika ukurasa huu kuna watu wa kada na taaluma mbalimbali naomba kwa wale wenye weledi juu ya kanuni za kikokotoo cha mafao ya wastaafu atutumie kanuni hiyo ili iwe rahisi kwa wanaotarajia kustaafu wajue kukomotoa mafao yao na kujua ni kiasi gani wanapaswa kupata.

Hili linatokana na sababu kwamba wastaafu wengi wanasubiri kitakachoongia kuwa ndiyo haki yao badala ya kufanya hesabu na kujua kiasi halisi hata kabla ya kuingiziwa.

Pili je ni kweli kuwa kikokotoo kipya kimeshaanza kufanya kazi kwenye mfuko mpya wa hifadhi za jamii wa PSSSF???? Hiii tunaweza kupata uzoefu kutoka kwa wale waliostaafu miaka miwili nyuma kama wamelipwa kwa kikokotoo kipya au cha zamani?

Wakuu naombeni radhi kwa mwandiko mbaya sina uzoefu mkubwa wa kuandika makala. Naombeni ushirikiano wenu
 
Mkuu umesoma au unajibu tu?
Ndio kichwa cha habari kimesema kimeanza kutumika lasmi na kama ulikusudia kuuliza basi umefanya kosa la kiuandishi la bila kuweka alama ya kiulizo mwisho wa kichwa cha habari
 
Kwa mujibu wa kichwa cha habari......ni kwamba unatuhabarisha kuwa kikokotoo kipya kimeshaanza kutumika lakini kwenye maelezo wewe tena unatuuliza sisi..........
 
Elimu ya Tanzania ni hatari sana!Yaani hata kuuliza swali huwezi?Hiyo heading yako ni taarifa na wala siyo swali!
 
Back
Top Bottom