Kikongwe amuua 'baby' wake kwa wivu

Fidel80

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2008
Posts
21,947
Reaction score
4,470
AJUZA mwenye umri wa miaka 70, Asha Omary mkazi wa Cha Ngedere, tarafa ya Ngerengere wilayani hapa, anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za mauaji ya mumewe, Rajabu Athuman (70) kwa kinachodaiwa kuwa wivu wa mapenzi.
Mauaji hayo yalifanyika Agosti 19, saa tisa alasiri, kijijini hapo, pale mwanandoa huyo alipochukua kisu na kumchoma mumewe mkononi na kusababisha kifo chake kilichotokana na kuvuja damu nyingi.
Source:Habari Leo

My take
Jamani wivu hauna umri, kupenda hakuna umri.
Poleni sana watoto, wajukuu na vilemba wa mzee Rajabu.
R.I.P Rajabu
 
Kweli kupenda ni mzigo..
R.I.P Babu Rajab Athumani!
 
Haya bhana Mzee wala hatumii viagra.............teh teht tehe....
 
sasa nae Rajabu kwa nini alicheza faulo mpaka Asha akajua.....ona sasa....
RIP Rajabu......
 
Inasemekana alijipatia kabinti kadogo bibi akashtukia dili
 
Fidel 80 ulivyoiweka thread kama mwandishi wa habari vile............

R.I.P Rajabu Mapenzi yanaua
 
Inasemekana ni raana ya ukoo. Maana eti hata shangazi yake huyo ajuza alimuua kwa stail ileile mme wake wakiwa wamekaa ndani ya ndoa miaka 54. Wanaotaka oa familia hiyo kuwa makini msije chinjwa.

Sourc: Jirani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…