Kikosi bora cha Eden Hazard: Messi na Ronaldo nje

Kikosi bora cha Eden Hazard: Messi na Ronaldo nje

poposindege

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
453
Reaction score
175
Mchezaji nyota wa timu ya Chelsea Eden Hazard ametaja wachezaji wake nyota watano huku akiwaacha wachezaji bora wa dunia Lionel Messi na Christiano Ronaldo.

Hazard aliulizwa juu ya kikosi chake bora na uefa.com ndipo alipowataja wachezaji watano bora kuwahi kutokea. Alimtaja Muargentina Juan Roman Riquelme na wabrazil Ronaldinho na Robinho.

Wengine ni washindi wa kombe la dunia na Ulaya wafaransa Thierry Henry na Zinedine Zidane.

Hakuchagua beki wala golikipa katika kikosi chake cha 'dream team'. Hazard anayehusishwa kuhamia Real Madrid wachezaji hao wote aliowataja watatu walichezea Real Madrid na wawili Barcelona.

Wengi wameshangazwa na orodha ya wachezaji wake kukosekanika kwa Lionel Messi na Christiano Ronaldo.

Chanzo:michezo365
 
Kupinga banch c.ronaldo kwa vitendo vyake vinavyoonekana mitandaoni vya kupakatwa
 
Kila mtu ana mtazamo wake. Yuko sahihi ingawa kumuacha Messi nje nayo ni mtihani
 
Alielewa swali tofauti na alilijibu kwa namna ya alivyolielewa hao ni wachezaji waliowika enzi hizo

Sasa sijui Cr7 na Messi mleta mada umewaingizaje ?? Umeacha wakina maradona na Pele unataja Cr7 na Messi

Huo ni uchochezi na ushabiki
 
Angeulizwa currently ni wachezaji gani anawakubari basi tungeshangaa messi na Cr7 kukoseakana ila swali lilihitaji wachezaji waliowahi kutokea

Mleta mada wewe ndo mwenye matatizo sio Hazard
 
Back
Top Bottom