Kikosi cha mizinga "block 41" - Tunasonga

ukwaju_wa_ kitambo

Senior Member
Joined
Sep 15, 2024
Posts
150
Reaction score
173
KIKOSI CHA MIZINGA - TUNASONGA

NImefungua macho kujikuta vitani/ kimenuka nadhani watu wameshafuta majani/ Epuka kujihami mabomu yana anguka jirani/ wanajuta kukuta haki haipatikani kwa Amani/ kuruta baki nyumbani tumevuka Imani/ Yaani kiasi kushuka dili ujistili ngizani / na bendera inaendelea kupepea nusu mlingoti/ wanajeshi na masela mahabusu nipe Riport.

Nipo tayari kukipaka hata mbele ya bwana mkapa/ nasio kama nadata ila ukweli unaomata / jeshi linaposonga hakuna wa kukamata/ adui wanaponiona vitani wanaufyata /.

Wanaosikia hawasikilizi/ wanaosikiliza hawasikii/ machizi sio miujiza/ tunasonga Namna hii/...
Kwenye nafsi ya kila mmoja...../ Na hii ni dhati / kurudi kwetu nyuma mwiko mpaka tujue tamati.

Chorus.

Tunasonga ..!!! Kwa mwendo wa farasi Au kinyonga

Endeleaaa....

Ukwaju wa kitambo
0767 542 202
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…