Kikosi cha Taifa stars chatangazwa

Shadida Salum

Journalist at JamiiForums
Joined
Sep 11, 2020
Posts
69
Reaction score
105


Kikosi cha Taifa stars kitachocheza michezo miwili ya kirafiki na Kenya tarehe 15 na 18 mwezi Machi. Mchezo wa kwanza wa kirafiki hautohusisha wachezaji wa Simba kwakuwa watakuwa na mchezo wa Klabu bingwa tarehe 16.

Baada ya kumaliza mchezo huo watakwenda moja kwa moja mpaka Nairobi kwa ajili ya mchezo wa pili wa kirafiki na Kenya. Kocha wa Taifa stars Poulsen ameeleza kuwa baadhi ya wachezaji hao wa Simba watacheza mda mfupi tu ili wapate mda wa kupumzika.

Baada ya michezo miwili ya kirafiki huko Nairobi Kenya Kikosi kitaelekea Equatorial Guinea kwa ajili ya mchezo mmoja kati ya miwili ya kufuzu Afcon dhidi ya Equatorial Guinea na Libya.

Mbwana Samatta atachelewa kujiunga na kikosi kwakuwa tarehe 21 atakuwa na jukumu kwenye Klabu yake hivyo ataungana na kikosi baada ya kumaliza majukumu yake.

Mchezo dhidi ya Equatorial Guinea utachezwa tarehe 25 na baada ya mchezo huo kikosi kitarejea tena kambini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa mwisho ambao utachezwa kati ya tarehe 28 au 30 mwezi machi.
 
Kenya tena!! Mbona serikali ya Kenya hivi karibuni iliwazuia wakimbiaji wake kushiriki Kili marathon...
 
WACHEZAJ WALIOITWA TIMU YA TAIFA NI ...

1 MANULA
2 KAPOMBE
3 TSHABALALA
4 KENNEDY JUMA
5 ERASTO NYONI
6 JONAS MKUDE
7 HASSAN DILUNGA
8 MZAMIRU YASSIN
9 JOHN BOCCO
10 HAMIS NDEMLA
11 SELEMANI MATOLA

tunaposema SIMBA NDIO TIMU YA TAIFA MUWE MNAELEWA*
 
Amenifurahisha kwa kualika vijana wa U20 ngoja tutengeneze timu kwa kuwekeza kwa vijana... Wakina Yondan, kaseja, Nyoni umri una waacha hivyo ni muhimu kuwaweka karibu na vijana waweze kuwaachia madini
 
Nilichokiona hapa ni wachezaji wa Simba wako 10 na wachezaji wa Yanga wako 7.
na nmemuona mchezaji ambaye amebakisha siku 4 amalize mwaka bila kufunga goli hata moja ligi kuu(VPL), alafu kaitwa Timu ya taifa..!!?
 
Kati ya hao 10, ni watano tu ndio wenye uhakika wa namba Simba, wengine wanatokea benchi
 
Toa Matola,
Waliobaki wote wawe first eleven ya Taifa. Tutabeba mpaka World Cup
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…