Kikosi Kazi: Tanzania ianze mchakato wa kupata Katiba Mpya baada ya Uchaguzi Mkuu 2025

Kikosi Kazi: Tanzania ianze mchakato wa kupata Katiba Mpya baada ya Uchaguzi Mkuu 2025

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa kilichoundwa na Rais Samia Suluhu leo kinawasilisha taarifa ya yake na mapendezo kwa Rais Ikulu, Dar es Salaam.

Kikosi kazi chini ya mwenyekiti wake, Rewakaza Mkandala kimependekeza Tanzania ianze mchakato wa kupata katiba mpya baada ya uchaguzi mkuu 2025.
======

Rwekaza Mkandala: Mwisho mheshimiwa Rais ni suala la muda mrefu, mwaka 2011 Tanzania ilianza mchakato wa kutunga katiba mpya kwa kutunga sheria ya mabadiliko ya katiba namba 83 ya mwaka 2011.

Oktoba 2, 2014 Bunge maalum la katiba lilipiga kura kupitisha katiba inayopendekezwa ambayo ilipaswa kupigiwa kura ya maoni na wananchi ili kuithibitisha lakini mpaka sasa suala hilo halijafanyika.

Changamoto mheshimiwa Rais ni mbili
  1. Kuna wale ambao wanasema hakuna haja kuwa na katiba mpya kwani katiba ya sasa inaweza kufanyiwa marekebisho kukidhi mahitaji ya sasa na baadae.
  2. Mchakato wa kupata katiba pendekezwa haukuwa shirikishi vya kutosha kwasababu baadhi ya wajumbe wa bunge la katiba walisusia hivyo katiba hiyo kupitishwa na wajumbe waliobaki.
Pia kuna madai mchakato wa kupata katiba mpya haujakamilika, umesimama muda mrefu tangu mwaka 2014 hivyo unapaswa kukwamuliwa.

Pia kuna maoni katiba pendekezwa imeacha mambo ya msingi yaliyomo katika rasimu ya katiba pendekezwa.

Pia kuna suala la katiba mpya kwamba ni muhimu lakini halina haraka kwakuwa katiba ya sasa inafanya kazi vizuri.

Kuna wale wanaosema kuna mahitaji mengi ya wananchi ya maendeleo kuliko uhitaji wa katiba mpya hivyo ni vyema kutumia muda huu kujikita katika kuleta maendeleo ya wananchi.

Mwisho kuna wale wanaodai katiba mpya sio suluhisho ya kila changamoto zinazotukabili, zipo nchi zinazosemekana kuwa na katiba nzuri lakini bado kuna malalamiko kuhusu masuala kadhaa ikiwemo masuala ya uchaguzi.

Hapa suala la kufanyiwa kazi mheshimiwa Rais ni kupendekeza utaratibu wa mchakato wa kutiba mpya na muda wa kufanyiwa kazi.

Kikosi kazi kinapendekeza kwamba Tanzania ianze mchakato wa kupata katiba mpya mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025. Mapendekezo ya namna mbalimbali ya kushughulika na suala la katiba mpya baada ya uchaguzi mkuu wa 2025

Pendekezo linatokana na sababu kuu nne
  1. Kuna haja ya kuainisha dira kuu ya maendeleo kwa miaka ijayo itakayotoa muelekeo kwa katiba mpya.
  2. Kukosekana kwa muda wa kutosha kuanza kutumia katiba mpya ndani ya kalenda ya uchaguzi wa 2025
  3. Kuna haja ya kutoa fursa kwa marekebisho ya sheria ya uchaguzi na sheria ya vyama vya siasa.
  4. Kuna haja ya kutoa fursa ya kutosha kufanyia kazi masuala ya muda wa kati ikiwa ni pamoja na kuanisha dira mpya ya maendeleo.
 
Ubunge au nafasi yoyot ya juu ikinyimwa mshahara na marupurupu makubwa ya kutisha, watoaji rushwa watakosa pa kukimbilia /maslahi makubwa ndiyo yanayovuta rushwa za kifedha na hata kingono nadhani hapa cdm wananielewa vizuri sana.

-tukumbuke si wanasiasa wote wanadhamira ya kutumikia watanzania almost 80% ni kwa ajili ya maslahi yao na familia zao.
 
Ubunge au nafasi yoyot ya juu ikinyimwa mshahara na marupurupu makubwa ya kutisha, watoaji rushwa watakosa pa kukimbilia /maslahi makubwa ndiyo yanayovuta rushwa za kifedha na hata kingono nadhani hapa cdm wananielewa vizuri sana.

-tukumbuke si wanasiasa wote wanadhamira ya kutumikia watanzania almost 80% ni kwa ajili ya maslahi yao na familia zao.

Lakini Mbowe kaprove tofauti
 
Hizi kamati za kijinga sioni sababu ya kuundwa zinapoteza pesa bure tu.

Ni ujinga zaidi kutegemea jambo la tofauti toka kwa mwanasiasa wa CCM anayeunda kamati ya maproffesor njaa makada wa lumumba, ije na majibu ya mahitaji ya watanzania.

Why isubiri baada ya 2025? kama sio wanafanya kazi kwa kumridhisha bosi wao aliyewalipa posho za hiyo kazi ya hovyo waliyofanya.
 
Hivi mbona hawasemi sababu ya kuhamishia baada ya uchaguzi wa 2025?

Suala la katiba mpya ni jipya hata lisubiri tena muda mwingine?

Hawa wajumbe wa hii kamati mbona kama ni wanufaika wakubwa wa katiba iliyopo?

Wanafikiri sisi wajinga, ila wajue tunajua ila tu hatuna nguvu ya kupinga, na hapa ndo wananufaika na katiba iliyopo. Hivyo hawa wanataka tuendelee kutokuwa na nguvu hivi hivi wao wakigawana hela zetu kwa vile katiba iliyopo inawapa nguvu hizo na sisi wananchi kutunyima.

Hakuna lolote la maana linaloweza kutokea kama katiba hii itaendelea isipokuwa waumiaji tutaendelea kuumia na wanufijaji hasa CCM wataendele kunufaika.

CCM hawawezi ridhia mabadiliko ya katiba hii kamwe!
 
Back
Top Bottom