Kikosi Kazi: Tanzania ianze mchakato wa kupata Katiba Mpya baada ya Uchaguzi Mkuu 2025

Hizi si ndiyo hoja za wana CCM na washabiki wao kwa miaka hii yote tokea 2014? Hata wangebadilisha kidogo lakini hivi zilivyo wamenakili na kuiita ripoti ya kikosi Kazi!

Ugumu Wa kupatikana Katiba mpya unakuwa upi? Nielewavyo Mimi kianzio ni rasimu ya Warioba,kuundwe timu ya wataalam huru,wapeleke mapendekezo kwa wananchi wapi pa kuboresha halafu liundwe Bunge Huru la Katiba ili tuandike Katiba mpya.Sifahamu kwa nini hawa wajumbe wameweza kuja na hayo mapendekezo kwa muda mfupi lakini tunashindwa hata kusogeza uchaguzi mbele kidogo kama kuna kukawia?

Hii maana yake kikosi Kazi kimetudharau sisi wananchi kuwa hatuwezi kukamilisha mchakato kabla ya 2025?
Je,hicho kikosi kilipewa hadidu za rejea zilizowaongoza hivyo?
 
Sasa hili swala linahaja ya kamati kweli,kamati zanyewe kama za kina manyele
 
Wanasiasa wasio na uchungu kwa maslahi ya wananchi ni wale Wa chama chakavu,na hiyo asilimia siyo sahihi maana ni zaidi ya 99% yao wapo kimaslahi.Kukataa Katiba pia ni maslahi binafsi na inadhihirisha jinsi walivyokuwa wabinafsi.
 
Vyama vya siasa vinapigwa pin kupeleka habari katika vyombo vya habari vya nje ya nchi.
 
Hatari sn
 
I 'm not late on board.

Kwa hii kamati ya makada wa CCM niwape watanzania pole tena ni danganya toto part II inakwenda kutokea.

Kama nia ipo basi wangeanzia pale walipoishia.

I
 
Huu ni USHAMBA. Mi nasema hivi, mchakato uanze sasa, halafu kura ya wananchi ya kuipitisha ipigwe sambamba na upigaji kura wa uchaguzi mkuu wa 2025 ili raisi wa awamu ijayo aanze kuitumia kuanzia 2026. Ina maana Rais Samia mwenyewe awe wa Kwanza kui- practice! Inamaana uchaguzi mkuu wa 2025 uendeshwe chini ya katiba ya sasa pamoja na marekebisho hasa ya sheria ya uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu. Hakuna haja ya kuwafanya na hofu maana haiathiri utawala wa mitano tena ya Mama Samia, labda vyombo vya ulinzi na usalama viamue vinginevyo maana tume ya uchaguzi ni kugonga mihuri tu!
 
Waache kuchezea akili za Watanzania. Miaka 4 kabla ya uchaguzi eti haitoshi. Kama miaka haikutosha tangu kwenye Tume ya Waryoba (2014) mpaka leo, basi tusubiri wajukuu wetu waje watengeneze katiba ya nzuri ya nchi.
Kukosekana kwa muda wa kutosha kuanza kutumia katiba mpya ndani ya kalenda ya uchaguzi wa 2025
 
Katiba ndio inazaa dira. Dira haiwezi kuzaa Katiba. Bila nguvu ya watu, nchi hii haiwezi kupata Katiba nzuri.
Kuna haja ya kuainisha dira kuu ya maendeleo kwa miaka ijayo itakayotoa muelekeo kwa katiba mpya.
 
Wezi wa kura wanataka waendelee kuongoza nchi kwa kura za wizi. Yule mama akisikia neno Katiba anaweweseka!!
 
''mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025''

....Ni lini hasa ? Maana hata 2029 ni baada ya Uchaguzi mwaka 2025.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…