Kikosi, Kikundi - Wataakamu wa jeshi karibu!

Kikosi, Kikundi - Wataakamu wa jeshi karibu!

Kipala

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2009
Posts
3,763
Reaction score
700
Salaam wenzangu hasa wataalamu wa habari za kijeshi. Naomba msaada kuhusu maneno kwa ajili ya vitengo ya kijeshi.

Kiingereza: Company, battalion, regiment, brigade, division, corps, army

Nasikia kwa Kiswahili ni company= kikosi, battalion = kikundi. Nauliza je: inaeleweka?
Maana kwa kugha ya kawaida wala kikosi wala kikundi ni idadi maalumu.
Lakini kwa lugha cha kijeshi "company" inaeleweka ni takriban watu 80-200, na battalion ni jumla ya company 2-7 yaani watu 500-1500.
 
Na mimi naomba niongezee msemo ulioibuka hivi karibuni baada ya maafa ya Mbagala. Nini maana ya msemo "kusafisha kambi" ?
 
Company, battalion, regiment, brigade, division, corps, army
knowledge ndogo niliyoipata wakti nikipita JKT kwa mujibu wa sharia, Nikiwa kambi ya Ruvu chini a Afande Meena wakti huo CO na capt Othman kamanda wangu wa A coy, walitufundisha kama ifuatavyo:

Company: hiki ni kikundi cha askari kinachoundwa na platuni tatu chini ya platuni kamanda. Sasa Company maana yake ni Kombania kwa kiswahili.

battalion: hii maana yake ni kikosi chini ya mkuu wa kikosi ambeye ni CO. battarion inaundwa na kombania tano au sita. Mfano ruvu tulikuwa na kombania a mpaka f kisha kulikuwa na HQ coy. Hivi viliunda kikosi cha Ruvu JKT.

regiment: hiki ni mikundi cha askari ( yaani wale wasio maofisa) katika kikosi. Nacho kinakuwa chini ya RSM ( Regiment surgin major)

Brigade: hii ni muungano wa vikosi katika kanda fulani na vinaongozwa na brigade commander.

Division: hii ni muungano wa vikosi vyenye kazi sawa. kama JKT vikosi vyote vikiungana wanafanya Division ya JKT nayo inaongozwa na Division kamanda, enzi zetu alikuwa Meja Gen Makame Rashid. Sijui Yupo wapi mtu huyu maana ake alikua mpenzi mkubwa saa wa taarab na ndie aliyeanzisha kikundicha JKT Taarabu chini ya Issa matona, Bia Hassan, Shakira Said n.k.


Dr Hamza.
Doha. Qatar


 
Back
Top Bottom