carlmax II
New Member
- Dec 31, 2021
- 4
- 2
KIKOSI MAALUMU CHA UFUATILIAJI NA UTEKELEZAJI.
Serikali iunde kikosi maalum cha kufuatilia utekelezaji na uwajibikaji wa watumishi serikalini na sekta binafsi. Kutokana na watanzania wengi kuwa wavivu na kutokuwajibika ipasavyo katika majukumu Yao, mifano michache ni kipindi cha awamu ya tano chini ya Hayati Rais Magufuli na kero nyingi zilizokuwa zinawasilishwa kwake azitatue aliyekuwa Mwenezi na mafunzo wa chama cha Mapinduzi ndugu Paul Makonda, kwenye mikutano yake.
Kuundwa kwa kikosi maalum kwaajili ya kufuatilia uwajibikaji na kuwawajibisha watumishi wazembe wasiotekeleza majukumu yao inavyotakiwa itasaidia kuwasimamia viongozi hao pia kuwaondosha kwenye utumishi wote wasiowajibika.
Kama ilivyo kwa usalama wa Taifa, lazima wapitie mafumo ya uaskari mfano JKT kwaajili ya ukakamavu na uzalendo. Kikosi kitakuwa chini ya Ofisi ya Raisi au Waziri Mkuu, na kipewe mamlaka ya kuamrisha vyombo vingine vya ulinzi na usalama Isipokuwa jeshi(JWTZ).
MATOKEO TARAJIWA KUTOKANA NA KIKOSI MAALUMU.
Kikosi hiki kitapunguza au kuondoa uzembe kwa waliopewa dhamana mbalimbali kwa kutambua wanafuatiliwa utendaji wao muda wote. Mfano barabara imeharibika au ina mashimo na mamlaka haifanyi ukarabati meneja wa TARURA AU TANROAD atashangaa anapigiwa simu kutoka ofisi ya Waziri Mkuu au wizarani na kumtaka kukarabati mara moja hivyo hawezi kujisahau.
Pia itakuwa njia ya kuondoa urasimu na kupunguza ukosefu wa ajira. Kwanza wale watakaopata fursa ya kuhudumu kwenye kikosi hiki maalumu watakuwa wamepata ajira hivyo kupunguza ukosefu wa ajira kwenye jamii ya watanzania hasa vijana. Pili kupitia ufuatiliaji wa utekelezaji Serikali itang'amua maeneo yenye upungufu wa rasilimali watu hivyo kuandaa mipango kwaajili ya ajira mpya ili kuleta ufanisi.
MUUNDO.
Muundo wa kikosi ni kwa ngazi ya Taifa hadi Wilayani. Hivyo watumishi wa kikosi watapatikana kita wilaya, ambako huduma na miradi mbalimbali hutekelezwa. Kazi ya kikosi ni kufuatilia utekelezaji wa miradi mbalimbali kwa kuzingatia thamani ya pesa, huduma muhimu kama Elimu, Afya, Ardhi, Rushwa, Uharibifu wa mondombinu na Uhujumu uchumi.
Mara panapobainika uzembe kwenye hayo maeneo wanaamrisha mamlaka husika kama TAKUKURU, POLISI, TFDA, TANAPA na nyinginezo kuchukua hatua stahiki.Pía kuwe na mawasiliano rasmi mfano namba za simu itakayomuwezesha mwananchi kupeleka taarifa moja kwa moja ngazi ya Taifa na taarifa hizo kufanyiwa kazi mara moja, kama kama mfumo wa huduma za dharura wa Tanesco.
Mfano watumishi wengi serikalini na mashirika binafsi hawahudumii wateja wao au wahitaji huduma vile inavyostahili. Iwapo kutakuwa na nafasi ya watanzania kutoa taarifa kwa njia za kidigiti kuripoti madhaifu hayo ili hatua stahiki ichukuliwe.
MATARAJIO YA MATOKEO.
Pesa nyingi za miradi zinafujwa kwenye Serikali za mitaa kwa kukisiwa gharama za juu zaidi kwa makusudi na utekelezaji wa miradi huwa chini kabisa ya kiwango. Iwapo mtandao wa kikosi au mawasiliano yatakuwepo hadi ngazi za vijiji hadi mitaa, itasaidia sana kuokoa fedha zinazofujwa na wasimamizi waroho. Sambamba na hilo miradi inayotelezeka itakuwa katika kiwango tegemewa na itadumu kwa muda uliotarajiwa.
Hii itawezesha watanzania kufanya kazi kwa uweledi na Kutoa huduma stahiki ndani ya miaka 10 hadi 20 jamii itabadilika na hadi kufikia miaka 25 yale mazoea ya kutokuwajibika ipasavyo hayatakuwapo tena ndani ya jamii ya watoa huduma mbalimbali. Hii itapelekea kila mtanzania kufanya kazi kwa bidii na kukuza uchumi wa nchi.
Kuwajibika ipasavyo kutaleta uzalendo pia kuondoa urasimu na Rushwa kwenye jamii na hivyo watu stahili watafanya majukumu stahiki hivyo weledi utatamalaki na kila jambo litatendeka kwa ustadi. Nchi itakuwa imepiga hatua kwenye kila sekta na kuwa kioo kwa nchi nyinginezo za Afrika na Duniani kwa ujumla.
Kuzuia urasimu, Rushwa, Ubadhilifu na uzembe kutaleta mapinduzi na uchechemuzi kwenye sekta nyingine za kiuchumi kama vile utalii, madini na teknolojia. Hii itasababisha ubunifu na matumizi ya teknolojia kwenye nyanja nyingi sana hivyo kukuza sekta hizo na mapato yake.
Tunategemea sekta binafsi zitaimarisha shughuli zao na kukuwa zaidi. Sekta binafsi na za umma zikishamiri zitakuza biashara na mauzo ya nje na kuongeza fedha za kigeni nchini. Kuongezeka kwa mauzo ya nje kutafanya uchumi wa Nchi yetu uwe imara zaidi.
Makusanyo ya kodi yatakuwa makubwa kutokana na viwango vya kodi kuwa rafiki bila kuumiza walipaji wa kodi. Hii itatanua usambazaji wa huduma za kijamii kama maji, Afya, Umeme na miundombinu ya barabara na reli. Mishahara ya watumishi wa serikali na wale wa binafsi itakuwa ya kuridhisha hivyo kufanya maisha ya kila mtanzania kuwa bora.
Kikosi pia kitasaidia kufuatilia uwajibikaji wa idara za kudhibiti magendo na biashara haramu kama usafirishaji wa Binadamu na ujangili kwenye mbuga zetu za wanyama. Pia kuhakikisha watanzania wanatumia bidhaa zenye viwango zilizothibitishwa. Suala la utunzaji wa mazingira pia litafuatiliwa ili kuhakikisha fedha zinazotolewa kwaajili ya kampeni na hatua za utunzaji wa mazingira zinafanya kazi iliyokusudiwa.
Naiona Tanzania iliyosalama na iliyoendelea baada ya miaka 20 hadi 25 kama KIKOSI MAALUMU CHA UFUATILIAJI NA UTEKELEZAJI kikiundwa na kupewa jukumu la kufuatilia uwajibikaji na utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya kiserikali na mashirika au makampuni binafsi.

Upvote
1