Kikulacho ki nguoni mwako, RIP Magufuli

Ni mapema kumjudge mama kuhusu misimamo yake na magufuli. Mi naona yuko committed kwa course ya magufuli huenda hujamuelewa tu. Pia ujue style ya mama itatofautiana. Mi hofu ni opportunists na majasusi wa ubeberu kumpotosha. Tuombe mungu mama aweze kuhimili mawimbi kutupeleka kwenye vision ya magufuli.
 
Makamu ni team Chato ambayo imedhulumu sana watu. Dhuluma siyo njia ya Mama. Lazima watatofautiana tu.
 

Mkuu nadhani unasahau mapema sana ,unakumbuka hotuba ya JPM wakati anazindua bunge? Uliona alivyokuwa anamponda JM Kikwete? Halafu kumbuka kwamba JIWE alikuwa hakubali ushauri rejea Makamba Snr alivyosema...Kutokubali ushauri ndio maana wasiadizi wake wakaamua kumlamba kisogo tu.

JPM alisema kabisa watu walikuwa wanashinda nje ya nchi kuliko kutembelea kijijini kwao,watu walikuwa watumia mabilioni kwa ajili ya matibabu ya nje tu,alikuwa anampa za chembe JK waziwazi,mwache na yeye serikali yake isemwe.
 
Mbona mwendazake yeye kutwa kuwasema na kuwananga watangulizi wake kana kwamba hakuna lililofanyika kabla ya Awamu ya Tano ni kama nchi ndio imepata uhuru wake 2015 chini ya Mtukufu Mwenyeheri Mwendazake John pombe Joseph Magufuli.


Waingereza wanamsemo wao kuwa "Muosha Huoshwa"
 
Ndugu yako alikuwa hashauriki, uzuri alikiri kwa kinywa chake mwenyewe hili!!!
 
Mama alikua na wakati mgumu sana kufanya kazi na yule mtu, yani nae atakua ameteseka kama sisi wananchi wa kawaida.

"mimi sio mtu wa kushauriwa, tena ukinishauri ndio unaharibu"

JPM- shujaa wa zamani.
 
Si kasema alikua ana solve ikamshinda?
Huyo magufuli alimshinda mama like!
Ndio maana alivopata nafasi lazima afatilie,
 
Mimi huwa nachukia sana mtu anaebishana na ukweli/uhalisia kama wewe mleta mada.

Mwenda alikuwa dictator/tyrant hakutaka kusikiliza ushauri wowote ndio maana hata waliomzunguka ikabidi waende nae kinafki tu ili kulinda ugali na familia zao.

Sasa kaenda inabidi turudi kwenye maisha yetu ya kawaida sio kukaa kinafki tena.
 
kuna washauri wanamshauri mama pengine wanamshauri hivi ila nasema tu kufuta legacy ya JPM ni miaka 100 labda
Mkuu, kuna msemo unasema....people will never forget how you made them feel...unapoongea kuhusu legacy....kuna ka ukweli kuwa hayati hatasahaulika...ila atakumbukwa kwa jinsi alegacy yake ilivyosababisha anaekumbuka kufeel...

#ukinizingua....shauri yako!
 
Wewe unaonekana ni miongoni mwa hao unaowaita Backbiters. Huyo unayemtetea mwenyewe kwa kinywa chake aliwahi kutamka kwamba yeye huwa hashauriwi/hashauriki na atakaposhauriwa ndiyo anaharibu kabisa.Nadhani ile Siku ndipo alipojibatiza jina lake maarufu la Jiwe.
Hata hivyo sikubaliani nawe kuwa Mh.Rais wetu ni Backbiter kama unavyotaka tuamini.Usimfunge kwenye kutimiza matamanio ya Mwendazake,akikubali ushauri wako inamaana hatofanya Yale anayoona yanawafaa Watanzania kwa sasa.Huyo ndiye Rais wa JMT wa sasa na jina lake Samia Suluhu Hassan hivyo atatenda Yale tu atakayoona yanatufaa zaidi Watanzania kwa wakati huku.
Busara inatutaka tumwache Mh.Rais wa JMT SSH aweke Legacy yake na mwendazake kama hakutumia muda wake vema siyo issue ya Rais wetu wa sasa.Mwenda zake alipiga chini tena kibabe miradi ya waliomweka madarakani(Watangulizi wake) na kuwaonya waache kuwashwa washwa.Miradi mizuri mizuri akaizindua upya na mlimsifia sana,kulikoni wa sasa mumpangie cha kufanya?
 
Mleta mada nenda ukapitie hotuba na kauli za jiwe kipindi alipoingia madarakani jinsi alivyokuwa akiuponda uongozi wa mtangulizi wake Kikwete ili hali alikuwa katika baraza lake la mawaziri akiwa waziri wa ujenzi . Mimi naona Mama yupo sawa kusema waziwazi mambo ambayo yaliyokuwa sio sawa kwa mtangulizi wake.
#jamhuri ya muungano wa Tanzania kazi iendelee
 
Wakati mama anazungumzia miradi,kuna mahali alisema kuna miradi mingine ipo kwenye makaratasi sijui itawezekana ila nataka niione.Hivi alikuwa na maana gani?.

Mayanga Construction tayari mmeingia woga !

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…