Kikulacho ki nguoni mwako, RIP Magufuli

Mkorosho ni mti ambao ndiyo ninaweza kuufananisha na utawala huu wa awamu ya tano na ya sita. Kutokana na kilimo hiki cha korosho kuletewa mizengwe mpaka ikafikia wakulima waone kama wamedhulumiwa kwenye mazao yao, mwisho hata kwenye vikatuni vikimchora mtu kama anakichwa cha korosho. Lakini ukweli mama Samia ndiye mwenye bahati ya korosho, kwani korosho huwa ni kikonyo kinachokaa chini ya tunda la nini kwa bahati mbaya bibo huwa halina thamani kutokana na asili ya ladha yake ya ukafu, ukilila mara linakupalia na kukusababishia kikohozi na kitu cha mwisho watu hufanya Pombe ambayo baadhi ya walevi huitumia. Lakini korosho ndiyo yenye thamani na yenye faida hata katika mwili wa binadamu. Hivyo awamu ya tano ni ilikuwa ya bibo lenye lutengeza Pombe na awamu ya sita ni ya korosho iliyotokana na bibo. Hivyo tutegemee kupata faida kama vile korosho inavyoleta faida kama zao la biashara na chakula chenye kirutubisho mwilini.
Kwa jina la jamhuri ya muungano.
Kazi iendelee.
 
Wewe NI MFUASI WA MWENDAZAKE naona Una machuungu!
 

Sitaki kuhukumu. Lakini inshu ya jinsi kigogo alivyokua anapata habari za ndani za ikulu.
 
Nakuunga mkono Kwa masikitiko na majonzi makubwa,lkn mungu yupo,wale aliokuwa ametuteua na kutuamini,leo hata 40 yake bado tunaanza kumtukana,ni jambo la kuumiza na kuhuzunisha sana,
 
Hivi kama mama alikuwa anashauri ila hasikilizwi alikuwa afanyaje zaidi.!?
Ni kukaa kimya na kuiangalia tu... Kheri liende hakutaka ugomvi.....

Sasa yeye ndio kayashikilia hayo maamuzi kwa aslimia Mia....

Acha mama aseme. Sijaona unafiki wake
Kitu gn kilikuwa kinamfanya alie samia,nini kilikuwa kinamfanya ahuzunike na kuuliza?,samia alikuwa akicheka na kupiga vigeregere,mungu yupo,kama kuna kundi lilihusika kumwangamiza jpm,kwa machozi na majonzi ya watanzania,wengi...
 
Maza nae asituzingue anatakiwa afate ilani ya chama cha mapinduzi yenye kurasa 303
 
Kaa kimya peke yako[emoji849] nilikaa kimya kumuombea mdogo wangu, inatosha.
 
Kwani Mwenzetu upon Nchi gani,huyo Mama alikuwa aachie ngazi toka kitambo sababu walikuwa hawapikiki yeye na Magufuli,bahati nzuri tu akina Mkapa na Kikwete wakamshauri akarudi.
Sasa mwenzetu unataka aendelee na kile kile ambacho alikuwa hakitaki.

kama ilikuwa hivyo maana yake urais hauwezi sasa.

makamu unajiudhuru kwa kushindwa kazi!!!!ni kazi ipi ataiweza kwa sasa na hana wa kumpelekea ripoti??

twende,wa kwanza kucheka atakuwa wa kwanza kulia pia.
 
Kwa hiyo ulitaka waendeleze Mambo ya kipumbavu ya magufuli

Yaani mtu anauliza kaa Nini hamna chanjo ya ukimwi

Hajui kabisa antigenic variations /strains za HIV
Au lentivirus anaropoka tu maskini
 
Safi Sana ponda huyo Jiwe maana ndivyo alikuwa anafanya kwa wenzio kea kujifanya yeye ndio ana akili Sana kuliko watangulizi,aende zake
 
Tafsiri nyingine ni kuwa Mama hakuwa anashirikishwa, yaani ilikuwa jeshi la mtu mmoja.
 
Hivi wewe unayelalama hapa unafahamu tabia ya Jiwe?Huyo mtu alikuwa hashauriki,unapomlaumu mtu yeyote kuhusu Jiwe unakosea sana.Jiwe alishajitaja kwamba yeye ni kiongozi wa malaika!
 
Kwa sasa watanzania hawawezi kukuelewa kwa kuwa wanamahaba! yaani ni zaidi ya mwanaume wa kipogoro na mndamba kukutana na utandu wa wali.
wacha muda utaeleza!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…