Kikulacho ki nguoni mwako, RIP Magufuli

Dereva na konda wanatakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano. Ila maamuzi ya mwisho ya gari iendeshwe kwa namna gani anayo dereva. Konda hawezi kulaumiwa kwa sababu ya dereva kuingiza gari mtaroni.
 
Na saizi wengi wa wateule wa Jiwe amewaweka kuwavutia mda tuu ,wakiteleza unapigwa chini mazima ndivyo alivyofanya kwa wateule wa JK,ngoja mama awe Mwenyekiti wa chama afute wote
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38] nimeipenda hii
 
nyinyi kenge mtakuwa wa kwanza kupiga yowe,tunawajua vyema.
MATAGA utapata tabu sana. Ulizoea kuishi maisha ya unafiki na kujipendekeza! Ila kwa sasa umebakia njia panda. Baadhi ya Mataga wenzako wameamua kuanzisha kambi isiyo rasmi ya upinzani kumpinga MAMA!

wewe unamanga manga tu humu! Nyambafu!!
 
Kwa kaliba ya mtu kama raisi Magufuli mtamuita mama samia mnafiki kwakumuonea,Magufuli aliongoza nchi kibabe kwakujiona yeye ni alfa na omega,Magufuli alikuwa na dharau kwa viongozi wenzake isio elezeka,watu wanakufa kwa korona raisi hataki wataalamu japo kuwaambia wanandugu wajue mpendwa wao amekufa kwa korona,
Biashara zinakufa raisi hastuki,Mungu anamakusudi yake kumtwaa huyu mtu mapema,
Nchi iliendeshwa kwa kauli ya mtu mmoja,
Ulikuwa utawala wakishamba Sana.
 
Ndio "utaratibu". JPM aliponda waziwazi mambo mengi ya JK na wengine waliomtangulia.
 
Yaani wewe uko kichwani mwangu, nawaza iweje mtu alifanya nae kazi ila yote walofa nya wote leo hayafai.
Kwakweli mm ni kati ya watu walioumizwa na kifo cha jpm nimeumia saaaana.

Nikawaza dk zake za mwisho atakuwa aliumia sana maana alijua haya yote yatatokea.

Wiki ijayo naenda chato. Nikamlilie kwa mara ya mwisho.sikubahatika kwenda mazishini. Maana naona maumivu hayaishi.

Kikulachooooo.
Rip jpm.
 
Watu wenye akili fupi hawawezi kuona impact ya Magufuli leo hiii....but time will tell
Ni wachumia tumbo, wanafii na watanzania wenye upeo mdogo wa kufikiri pekee, ndiyo wanao mkubali magufuli! No time will tell for magufuli! That is the reality!! He was the worst president!
 
pole kwa maumivu mkuu, bt kwa bandiko lako unahitaji neno la faraja

kikwete alisemwa sana na mwenda zake kwa madudu ya utawala wake bt legacy yake ipo pale pale, hata mwenda zake legacy yake itabaki hata kama MAMA atabeza.
 
Kwani Mwenzetu upon Nchi gani,huyo Mama alikuwa aachie ngazi toka kitambo sababu walikuwa hawapikiki yeye na Magufuli,bahati nzuri tu akina Mkapa na Kikwete wakamshauri akarudi.
Sasa mwenzetu unataka aendelee na kile kile ambacho alikuwa hakitaki.
Acha hekaya za kigogo wewe!

Yani alitka kujiuzulu kisha 2020 akakubali tena kuwa makamu rais?

Hivi huwa mnafikiri kila mtu ni mjinga?
 
Nakuunga mkono Kwa masikitiko na majonzi makubwa,lkn mungu yupo,wale aliokuwa ametuteua na kutuamini,leo hata 40 yake bado tunaanza kumtukana,ni jambo la kuumiza na kuhuzunisha sana,
Urais huu ni matokeo ya ajali ya kikatiba. Utasababisha maumivu makubwa sana kwa taifa.
 
kuna washauri wanamshauri mama pengine wanamshauri hivi ila nasema tu kufuta legacy ya JPM ni miaka 100 labda
Legacy gani ,ya ukabila? Kuvunja katiba au kuiba trillion 1'5? Au kubomolea nyumba watu ubungo, kumara? Au legacy ya kuteka na kupiga risasi watu? Huyu mwehu angekuwa nchi zinazojitambua asingeongoza hata miezi sita angeondolewa the guy was a disgrace thank you God for Divine intervation he is gone mwizi wa kura
 
Mama Yuko vizuri sana.
 
Kwa taarifa yako aliyokuwa anayafanya Magufuli hayakuwa yanastahili kufanywa na mtu ambaye ni rais. Usitake huyo mama aweke hadharani mambo ya huyo Magufuli maana hata ni aibu na fedheha. Mama ameamua kujitenga na tabia za mtu muovu. Kama ulikuwa unamuona kuwa anakosea ungeleta uzi wa kumkanya tabia zake. Subirini watu watoe mrejesho wa tabia mbaya za viongozi ili siku nyingine mkanyane mkiona mtu anakengeuka.
 
Ndugu yangu,akili ni nywele, kila mtu ana zake.
Huwezi kulazimisha akili za Mama Samia ziwe hizo hizo za Hayati Magufuli.
Kila mmoja ana maono yake.
Wewe umesikia wananchi wakilaumu?
Wewe una lako jambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…