Kikundi cha wanasayansi wa kimataifa kinasema kuwa homa ya mapafu ilitokana na waafrika

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Kikundi cha wanasayansi wa kimataifa
kinasema kuwa homa ya mapafu ilitokana na

waafrika waliokuwa wana hama hama miaka

70,000 iliyopita

Utafiti wa wanasayansi hao bila shaka ni

kinyume na dhana kwamba homa ya Mapafu
ilitokana na wanyama miaka 10,000 iliyopita na
kusambaa hadi kwa binadamu.

Utafiti huo unaonyesha uhusiano mkubwa ulioko

kati ya historia ya binadamu na homa ya
mapafu au TB.

Ugonjwa huo husababisha zaidi ya vifo milioni
moja kila mwaka.

Utafiti wa awali ulionyesha kuwa homa ya
mapafu ambayo huwaathiri wanadamu ilianza
kusikika tu miaka 10,000 iliyopita wakati idadi ya

watu ilipoanza kuongezeka huku wengi wakianza
kufanya kilimo.

Watafiti walikusanya taarifa za kijiografia na data
kuhusu genetiki za watu kutoka kwa aina 259 ya
vimelea vya homa ya TB kwa lengo la
kufananisha na historia ya binadamu Afrika.

Profesa Sebastian Gagneux, kutoka katika taasisi
ya magonjwa ya kiafrika nchini Uswizi alisema
kuwa , walichogundua ni kuwa binadamu wa

kwanza alitokea Afrika sawa na maambukizi ya
kwanza ya Kifua Kikuu kuripotiwa miaka 60,000
iliyopita , ikisemekana kuwa mapema mno
ikilinganishwa na ilivyodhaniwa.

''Lengo letu ni kutaka kuthibitisha kuwa ugonjwa
wa kifua kikuu ulianza kuenea miongoni mwa
binadamu na baadaye kuenea kwa wanyama,''
alisema Profesa Sebastaian.

Swali sasa ambalo wanasayansi wanahoji ni vipi
vimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu viliweza
kudumu kwa miaka 60,000 miongoni mwa watu
wachache sana.

Moja ya mambo yanayowashangaza wanasayansi
ni kuwa mtu anaweza kuambukizwa ugonjwa
huo kwa miaka mingi kabla ya kuanza
kuonyesha dalili za kuambukizwa.

Hali ya ugonjwa huo kukaa kwa miaka mingi bila
ya kuonyesha dalili ndiyo inawafanya watafiti
kuamini kuwa sababu kuu ya ugonjwa kudumu
kwa muda huo mrefu.

Wakati idadi ya watu ilipoanza kuongezeka
ugonjwa huo nao ukaanza kusambaa.
Na wakati watu walipoendelea kuongezeka
ndiposa ugonjwa huo nao ulipoendelea kuenea.

Hatua itakayofuata katika utafiti wa wanasayansi
hawa ni kutumia data ya jenetiki kuelewa
ambavyo vimelea vya TB viliweza kudumaa kwa

miaka mingi kabla ya kujitokeza kama ugonjwa
mwilini mwa mtu.

Ugonjwa wa Kifua Kikuu ni tisho kubwa duniani
kwa kusababisha vifo milioni 1.4 mnamo mwaka
2011, kulingana na shirika la afya duniani.

Ikiwa wanasayansi wanaweza kuelewa uhusiano
uliokuwepo kati ya ugonjwa wa TB

wanadamu,inaweza kusaidia katika juhudi za
kupunguza maambukizi yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…