Shule ya Msingi ya Kikuyu inayopatikana Manispaa ya Dodoma (Mjini) wanafunzi wa shule hiyo wanakaa chini kwenye sakafu. Waalimu wa shule hii wanawaagiza watoto kufika na mifuko ya salfeti ili wawe wanakalia wakati wakiwa darasa mda wa masomo.
Hii nimeishuhudia siku ya leo asubuhi ndipo nikaamua kumhoji mtoto mmoja jinsia ya kike darasa la tano (V), na nikapewa majibu kuwa waalimu wao wanawaagiza wafikapo shuleni wanatakiwa wanaende na mifuko ya salufeti (magunia) kwa ajili ya kukalia. Jamani elimu hii tutaishia wapi nayo?