MaxShimba
JF-Expert Member
- Apr 11, 2008
- 35,771
- 4,065
Ibara inayohusiana na uhuru wa kuabudu, ina utata mkubwa. Utata huu, unasababishwa na upungufu wa tafsiri. Utata huo utazua mtafaruku mkubwa baina ya makundi ya kiimani na vyombo vya dola, pale vyombo hivyo vitakapokuwa vikiingilia taratibu za dini hizo kwa kuzitafsiri kuwa ni kashfa.
Ibara hiyo inasomeka hivi: 31.-(5) Ni marufuku kwa mtu, kikundi au taasisi ya dini kutumia uhuru
wa kutangaza dini kwa kukashifu imani na dini nyingine, kujenga chuki au
kuchochea vurugu na ghasia kwa madai ya kutetea imani au dini.
Vyombo vya kutafsiri sheria, vimekuwa vikipata ugumu wa kupata tafsiri sahihi kuhusiana na neno kashfa, au kwamba ni kitendo gani kinapofanyika huhesabika kuwa mtu ametenda kosa la kukashifu.
Neno kashfa lina asili yake kutoka katika lugha ya Kiarabu.Maana yake funua kilichofunikwa.
Katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu uk.147 neno kashfa limetafsiriwa kuwa ni :- "ufunuaji au udhihirisho wa jambo la aibu; na Kashifu ni:- kutoa nje siri ya jambo la aibu; nyambua 2. jua au fahamu jambo la siri la moyoni mwa mtu mwingine kabla mwenyewe hajalieleza."
Maana ya wazi zaidi ni mfano wa mtu mume anapofunua maungo ya mwanamke asiye mke wake. Tendo hilo ndilo linalokamilisha tendo la kashifa kwa maana ya kufunua jambo la aibu.
Tendo la kusema kinyume na imani ya dini linaitwa kukufuru na wala siyo kukashifu. Neno kukufuru halimo katika rasimu ya Katiba hii.
Hili litaleta changamoto kubwa katika imani zetu. Kwa mfano baadhi ya vitabu vya dini vinataja kwa uwazi habari za watu wa dini zingine. Mfano Qur'an Tukufu inataja habari za Wakristo mara 62. Ikiwa neno Kashfa litatafsiriwa kuwa ni uchochezi, itabidi aya hizo 62 zilizomo ndani ya Qur'an zifutwe ili kuwaepusha Waislamu na vifungo kutokana na uchochezi.
Pia itabidi kila Muislamu anaposoma aya za Qur'an anapofikia aya zile zinazotaja watu wa dini nyingine mfano Wakristo na Wayahudi, aziruke ya hizo ili kuepuka kufungwa.
Hili litaleta mfarakano zaidi badala ya kuleta utengamano. Tulirekebishe mapema.