Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 302
Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma kimeshindwa kutoa sababu za msingi juu ya nini kimemsibu mgombea Urais wa Chama hicho hadi kuamua kuahirisha ziara yake aliyotakiwa kuifanya katika wilaya tatu za mkoa huu.
Kwa mujibu wa ratiba kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, mgombea wa Urais wa CCM , Jakaya Kikwete alitakiwa kufanya ziara katika Wilaya za Mpwapwa,Chamwino na Dodoma Mjini akitokea Kondoa ambako alimaliza ziara hiyo juzi.
Mgombea huyo alifika uwanja wa ndege wa Dodoma Mjini akitokea Kondoa na kupokelewa na umati mkubwa wa wanachama wa CCM, lakini ghafla jana alilazimika kuondoka na kuelekea jijini Dar es Salaam.
Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma John Balongo aliliambia gazeti hili kwa njia ya simu kuwa mgombea huyo ameamua kuelekea jijini Dar es Salaam.
Habari zilizopatikana kutoka kwa baadhi ya viongozi na wagombea wa nafasi mbalimbali zilieleza kuwa kiongozi huyo aliamua kuondoka baada ya kubaini kuwa Wilaya ya Dodoma mjini bado ina mpasuko wa kisiasa.
Rais alisema hawezi kuhutubia katika mikutano ambayo wagombea wake hawajawa kitu kimoja kwa hiyo akataka wayamalize kwanza ndipo atarudi kwa ajili ya kuendelea na kampeni alisema mmoja wa viongozi ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe.