Elections 2010 Kikwete aahirisha kampeni Dodoma

Luteni

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
2,274
Reaction score
302
Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma kimeshindwa kutoa sababu za msingi juu ya nini kimemsibu mgombea Urais wa Chama hicho hadi kuamua kuahirisha ziara yake aliyotakiwa kuifanya katika wilaya tatu za mkoa huu.

Kwa mujibu wa ratiba kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, mgombea wa Urais wa CCM , Jakaya Kikwete alitakiwa kufanya ziara katika Wilaya za Mpwapwa,Chamwino na Dodoma Mjini akitokea Kondoa ambako alimaliza ziara hiyo juzi.

Mgombea huyo alifika uwanja wa ndege wa Dodoma Mjini akitokea Kondoa na kupokelewa na umati mkubwa wa wanachama wa CCM, lakini ghafla jana alilazimika kuondoka na kuelekea jijini Dar es Salaam.

Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma John Balongo aliliambia gazeti hili kwa njia ya simu kuwa mgombea huyo ameamua kuelekea jijini Dar es Salaam.

Habari zilizopatikana kutoka kwa baadhi ya viongozi na wagombea wa nafasi mbalimbali zilieleza kuwa kiongozi huyo aliamua kuondoka baada ya kubaini kuwa Wilaya ya Dodoma mjini bado ina mpasuko wa kisiasa.

“Rais alisema hawezi kuhutubia katika mikutano ambayo wagombea wake hawajawa kitu kimoja kwa hiyo akataka wayamalize kwanza ndipo atarudi kwa ajili ya kuendelea na kampeni” alisema mmoja wa viongozi ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe.
 
duuuu, yaaani wamalize wenyewe mpasuko au yeye ndiyo aumalize? hata hivyo kwani si anaenda kuomba kura zake kwa wananchi au anawaombea wabunge tu?
ila jana niliona kama ali officiate shughuli fulani y a kiserikali dar. naona ameshajichokea huyo ameamua akapumzike dar. anyway Slaa endelea kuchanja mbuga mtakutana na JK getini ikulu wewe unaingia yeye anatoka.
 
"... is it?!!..... ....Aiseeeeeeee!!" :confused2:
 
si ajabu yuko hoi bin taabani, mficha maradhi.......
Halafu cha kushangaza ni kwamba umma wa Watanzania unafichwa ukweli ni nini hasa kinachoendelea. Si tuliambiwa kwamba jamaa atafanya kampeni usiku na mchana bila kulala!!! Kulikoni tena? Zikiwa zimebakia wiki sita tu na hali ya kushinda imegubikwa na wasiwasi mkubwa miongoni mwa mafisadi kuna neno kubwa hapa ambalo linafichwa.
 

Si imetangazwa kuwa aliahirisha kampeni ili kufungua mkutano wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu. Ambapo Jaji Augustine Ramadhani aliapishwa (mtanzania wa kwanza) pamoja na majaji wengine watatu kuwa majaji wa mahakama hiyo. Pia kushughulikia kazi nyingine za kiserikali. Baada ya hapo ataanza kampeni Iringa.
 
Kama sababu kubwa ingekuwa kufungua mkutano basi angerudi Dodoma kuendelea kulikoni kubadiri ratiba? kama anakwepa matatizo ya Dodoma na kukimbilia ya Iringa akifikiri ni mepesi anajidanganya.
 
Kama sababu kubwa ingekuwa kufungua mkutano basi angerudi Dodoma kuendelea kulikoni kubadiri ratiba? kama anakwepa matatizo ya Dodoma na kukimbilia ya Iringa akifikiri ni mepesi anajidanganya.

nafkiri jukumu la kumpangia ratiba ni la watu wengine katika kamati yake ! au wewe ni mwanakamati ulimshauri akakataa
 
kwani wewe utajua ratiba zote za watu au za vyama vyote vya siasa. mabo mengine ya kifamilia kama kuhudhuria mazishi kuona wndugu wagonjwa na hata maswala ya watoto zako au walw binadamu . Mbona tulishaona program nnyingi za viongozi huko nyuma zikikatizwa bila kutolewa sababu ya msingi. Msisimbue sana vichwa kwa maswala yasiyo na tija katika utatuzi wa shida za wananchi ambzozo ndio tungezipa kipa umbele kwa sasa.
Kama sababu kubwa ingekuwa kufungua mkutano basi angerudi Dodoma kuendelea kulikoni kubadiri ratiba? kama anakwepa matatizo ya Dodoma na kukimbilia ya Iringa akifikiri ni mepesi anajidanganya.
 
Takwimu za synovate na redet kuwa anapendwa zinamsaidiaje sasa?
very vere
 
kwa nini asiendelee alipoishia Dodomya anakimbilia ilinga Tiss WAMEMWAMBIA Iringapametulia?
 
Rais huyo huyo si ndiye mmemwona akifungua mkutano wa mahakama wa Afrika hapa Dar?

Pia alienda kuhani kifo cha mtoto wa Msekwa hapa hapa Dar? Sasa angelikuwa kwenye kampeni saa ngapi?

Kwa kuzua tumezidi, hii haina tofauti na wale wanaotangaza opinion polls ambazo hazipo.

Safari ya Iringa ilikuwa inajulikana tokea mwanzoni, hivyo kilichofanyika ni kuahirisha ratiba ya uchaguzi ya jana.
 
Tuache kulalama Muungwana mgonjwa kafanya mikutano mingi mwili umekataa lazima apumzimke.
 
Kamkimbia John Malecela! Atampamba vipi Lusinde mbele ya Malecela?
 

Kuna siri nilitaka niifiche lakini wacha nitoboe tu. Jamani eenh.......watu wa Ikulu si mnakumbuka alichosema Sheikh Yahaya kuwa atakaegombea kumpinga Kikwete kwamba itakuwa nini vile..... sasa Mwenyezi Mungu ile ilimkera sana na amepindua maneno ya Sheikh Yahya kwamba Kikwete akigombea.......... eenh.

Sasa mkitaka mumsevu jamaa inatakiwa yafanyike yafuatayo:

1. JK amkane Sheikh Yahaya hadharani mara moja.

2. JK aachie ngazi kama baadhi ya wagombea ubunge waliopewa rushwa na CCM walivyofanya na yeye aachie ngazi saa hii awaache wagombea urais wengine waendelee na mchakato.

Ni mambo hayo mawili tu yatamsevu huyu jamaa na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu....kwa sababu Ikulu chini ya JK na serikali ya CCM wamefanya ushirikina na kufuru.

Sasa mtachagua nani wa kumsikiliza......, mimi ninayewaandikia matakwa ya Mwenyezi Mungu au huyo Mchawi.
 
Kazi kweli kweli nasikia kaja Iiringa na ameamua aanzie kilolo maana apa town mtafaruku wa Mbega na Mwakalebela bila shaka wanamuandalia njia mbunge wa CHADEMA.
Ila huyu sheikh kwa nini Kikwete asimdenounce hadharani unaweza kuta ni kweli ni patner wake.
No wonder anaiendesha nchi kama gari bovu maana mungu kamweka pembeni kabsaaaaaaaaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…