Mpaka Kieleweke
JF-Expert Member
- Feb 27, 2007
- 4,132
- 1,577
Jana wakati Rais Kikwete akiwa anazindua komandi ya kikosi cha ardhini cha jeshi letu JWTZ aliutangazia umma kuwa ameamua kuongeza muda wa kustaafu kwa wanajeshi eti kutoka miaka 57 hadi miaka 60.
Sasa hawa ni watumishi wa Serikali na wapo chini ya sheria ya utumishi wa umma , sasa haya mamlaka ya kuongeza muda wa kustaafu ameyatoa wapi?
Ametumia kigezo gani cha sheria ama ni sheria gani inampa mamlaka ya kuongeza muda wa kikundi fulani cha wafanyakazi kustaafu?
Tunaelekea wapi na utamaduni huu wa kuvunja sheria za Nchi , na je?tukienda hivi tutaweza kufika?
Namshauri Rais sasa awe anafuata sheria na kamwe asiwe wa kwanza kuvunja sheria , na yeye ajue kuwa kama alimwadhibu Mnnali kwa sababu ya kuwacharaza waalimu bakora na kusema huko ni kukiuka sheria anapaswa naye awajibishwe .
Tujenge utamaduni wa kuheshimu sheria zetu, kwani Nchi bila sheria ni fujo.