Kikwete amkubalia Mwanyika kung'oka


Kumbe sisi wenyewe ndio tunawapalilia mafisadi halafu baadae tunakuja kujilaumu. Kama ulichosema ni kweli basi tutakuwa hatuna sababu ya kumtaka Kikwete na serikali yake kuwa wasafi. Mie nimechoka kabisa.

Kila mtu kwenye nafasi yake ajue kwamba halazimishwi kufanya kitu chochote asichokubaliana nacho. Kuna taratibu za kupinga na kupiga kelele, kujiuzulu ni hatua ya mwisho kbisa. Tusidanganyane eti nchi ingetingishika! Kama kweli ingetingishika basi wangekubaliana na uamuzi wako, kwa nini wewe ndio ukubaliane na uamuzi wao?? Lol!
 
Hayatabiriki. Tuliyaona kwa Gray Mgonja: alistaafu, yakafuata mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka. Tuliyaona hapo kabla kwa Omar Mahita: alistaafu, yuko nyumbani kwake analima mboga, hakuna anayemsumbua. Tuliyaona pia kwa Ben Mkapa: alistaafu, tukaambiwa 'mwacheni mzee wa watu apumzike'. Nchi yetu hii hii.
 
Bora waachwe wapumzike kama baba lao kuliko kusumbua fedha zaidi kuchezesha video za kina Mgonja zisizokuwa na tija. Wote wezi tu, hakuna mwenye uwezo, dhamira wala nia ya dhati ya kumwajibisha mwenzake.
 
..Mwanyika,Mwakapugi,na Mrindoko, walikuwa wanatekeleza amri za wakubwa zao tu.

..hata Dr.Mwakyembe analielewa hilo na ndiyo maana akasema kuna mambo ambayo Kamati yake iliamua yasiwekwe ktk ripoti ili serikali isiaibike.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…