Kikwete ampa neno Alikiba kuhusu ndoa yake

Kikwete ampa neno Alikiba kuhusu ndoa yake

MumbaZ

Senior Member
Joined
Jan 28, 2018
Posts
133
Reaction score
124
Rais mstaafu, Jakaya Kikwete amempa nasaha za maisha ya ndoa na ujana, Ali Kiba ambaye yuko kwenye harakati za kufunga ndoa hivi karibuni.

Ingawa taarifa za awali kutoka Mombasa zimekuwa zikieleza kuwa mwanamuziki huyo tayari ameshafunga ndoa na mrembo Aminah Rekish wa eneo hilo la mwambao, ujumbe wa rais mstaafu unatupatia mwanga zaidi kuwa tukio rasmi litafanyika hivi karibuni.

Ali Kiba amemtembelea rais huyo mstaafu nyumbani kwake. Hakutoka mikono mitupu, bila shaka ameongezewa busara zaidi za maisha.

Kupitia twitter, Kikwete ameweka picha inayomuonesha akiwa na Ali Kiba pamoja na mwanafamilia mwenzake wa RockStar 4000, Ommy Dimpoz katika picha ya pamoja iliyomjumuisha pia mama Salma Kikwete.

“Namshukuru @officialalikiba kuja kunitembelea na kunitaarifu kuwa anatarajia kuoa hivi karibuni. Nimempatia nasaha zangu na namtakia kila lakheri kwa jambo hilo jema aliloamua kufanya,” Kikwete ameandika.
 
Naona linapokuja swala la kuoa wasanii wetu wanavuka border. Ila kwa mademu wetu dizaini ya wema sepetu I think they are right
 
Ooow
JK, "hii ndio nn?"
Ommy, "hii inaitwa snap chat"
JK, "Snap chat?? siifahamu"
Ommy, "ooh niliwahi kukufundisha"

Lol, he is so sweet our former prezdaaa.

Hi mama Salma.
 
Kula waliwe wakina jokate,Madame rita etc ila kuoa waolewe watu wa mombasa, Shame on you wanawake wa bongo wakina wema sepetu uchi mmebaki kugawa tu kama wauza karanga.
 
Alikiba hongera sana kwa uamuzi uliochukua, hakika ndoa ni nusu ya dini, Mola awalinde.
 
Kula waliwe wakina jokate,Madame rita etc ila kuoa waolewe watu wa mombasa, Shame on you wanawake wa bongo wakina wema sepetu uchi mmebaki kugawa tu kama wauza karanga.
Wema anaolewa na Diamond.........Wa hapa hapa!
 
King kiba hongera sana

Hapo ndo ninapo mkubali kiba yaani ni vitendo dhidi ya maneno
 
hi game ukishaoa ndio tiketi ya kupotea..
 
Kula waliwe wakina jokate,Madame rita etc ila kuoa waolewe watu wa mombasa, Shame on you wanawake wa bongo wakina wema sepetu uchi mmebaki kugawa tu kama wauza karanga.
Hahahaha... Madam matalent bado anaita etiiiii...
 
Nimesikia dem anakaa Kenya na vile vile ni mtangazaji huko kenya.Hapa napo tuombe mungu tu maana Kiba nae silent killer aka zipu mbovu ,mtu uliozoea kugonga alafu mke wako yupo mbali ,lazima utachepuka tu.
 
Back
Top Bottom