Bubu Msemaovyo
JF-Expert Member
- May 9, 2007
- 4,120
- 3,468
Kama mtoto mchanga ajifunzavyo tabia za watu hususani wazazi wake kwa kuwaangalia sura zao, kuwasikiliza sauti zao huku wakilinganisha na matendo sambamba na sauti zao, ndivyo nilivyo ng'amua nia hasa ya Mh Rais JAKAYA MRISHO KHALFAN KIKWETE. Katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi, Mh. Rais alivinanga sana vyama vya upinzani. Katika hali ya kawaida wale waliosikiliza hotuba ile wakiwamo waandishi wa habari na wahariri walikuja na tafsiri zao na mitazamo yao wakiwa na lengo la kupigia debe magazeti yao yapate kununuliwa siku ile.
Haingewezekana Mh. Rais Kikwete kwenda kinyume na itikadi ya baadhi ya viongozi wandamizi wa CCM, lugha alizotumia kama vile "Lissu ni muongo, mnafiki na mzandiki" ni lugha ya kuwaridhisha CCM kuweza kukaa jamvi moja wakaendelea na "kucheza drafti lao".
Kitendo cha Mh. Rais kuwaita viongozi wakuu wa vyama vya upinzani pale Ikulu (Magogoni, ndicho kinachonisukuma kuamini na kushawishi jamii waamini kwamba nia ya Mh. Rais kama Kikwete binafsi ni nzuri na anapenda ipatikane katiba bora yenye lengo na maslahi kwa taifa. Mchakato wa katiba ni process ngumu inayohitaji umakini sana katika kuuandaa, wabunge makini wa vyama vya upinzani wameonyesha njia sahihi ambayo hata Mh Rais ameridhia. Bila upinzani Tanzania ni afadhali hata Rwanda ya 1994. Tuwe watulivu na wasikivu katika suala la kupata katiba mpya. Kwa upande wa CCM tambueni kwamba japo kobe huishi miaka mingi sana lakini hufikia muda akazeeka na kufa. CCM mmezeeka sasa kifo kipo kando ya mioyo yenu. Tulieni mpate madaktari waweze kuokoa japo mapafu yakaweza kufanya kazi muweze kuishi japo miaka miwili mkiwa madarakani.