Kesho rais atakuwa jimboni kwake, ni kweli mafisadi are attacking him form every corner of this earth, sasa hata watoto wake wanahitaji ulinzi kusafiri kutoka shuleni kurudi nyumbani,
Tunasema kwamba msimamo wa kiongozi siku zote hupimwa na kwa njia mbali mbali, lakini kiongozi shujaa kama Mwakyembe hufanya kama anavyofanya sasa, yaani husimama imara ingawa majaribio ni makubwa na magumu sana,
Tunamuombea yeye na wengine wote walioamua kumshika simba sharubu, Mungu awape uzima na maisha marefu kuliko ya mafisadi, na tunamuhaikishia Mwakyembe kwamba hauko peke yako, wananchi wengi tuko nyuma yenu.
Jumapili nilimbeba fisadi namba moja toka airport mpaka anakokwenda, amechoka kama mbwa, hakuweza kuniangalia usoni anaongea huku anakimbiza uso, ninasema siku zao zinafikia ukingoni, ninaamini kuwa kuna siku atalala hataamka maana amechoka sana, Shujaa Mwakyembe na Kubenea hakuna wasi wasi, maana baadhi ya sisi walalahoi wa got your back, atakayewagusa anatugusa na sisi, na bahati nzuri sana sisi walalahoi wengine hatuna anything to loose au to gain, kwa hiyo protecting you could be fun as well!
Angalieni mbele tu!
Mungu Aibariki Tanzania.