Huyu mtumishi wa Mungu nakubaliana nae kabisa kama kweli sie Watanzania tutakuwa kama huyu Mchungaji basi nchi yetu itakuwa mbele sana tu.Kwa maana hiyo basi tarehe 31 tukamchague yule ambae ameonyesha nia njema kutukomboa bila ya kujali dini wala chama.Mimi nasema watanzania ue uko nje ya nchi au ndani himiza familia yako jamaa zako majirani wakamchague yule mambae ameonekana una uchungu na nchi hii,Tukumbuke Elimu,maji,afya,makazi bora hivi ni vitu muhimu sana kwetu sisi Watanzania.Mwaka huu tujaribu kumchagua mtu na sio chama chake,maslahi ya nchi mbele chama baadae.Tusikubali wagombea ambao wanakumbatia Mafisadi na kuwanadi ka walipa kodi ati huyu ni mchapa kazi bora Hatudanganyiki.Kuna jamaa kauliza kama nani anayefaa kuwa Rais kwa upande wangu mie nasema Dr Slaaaa anaweza tumpe mimi mwenyewe ni Mpenzi wa CCM lkn sipo kichama mwaka huu niko kwa maslahi yetu na Taifa letu na mie mwenyewe na wewe ndugu pia,Inakuwaje tuachiwe madini ya Tanzanite baada ya shiriki kumaliza muda wake can u imagine inaingia akilini yaani washavuna na sie ndo tukakombeleze duuh.Kama tutawarudisha hawa jamaa tena itakuwa tumejipa laana wenyewe ya milele.*