Elections 2010 Kikwete avunja rekodi ya kukaa nchini

Rugemeleza

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2009
Posts
668
Reaction score
136
Ndugu zangu,

Napenda kutoa taarifa kuwa Raisi Jakaya Mrisho Kikwete hadi leo amevunja rekodi ya kuweza kukaa Tanzania bila kutoka nje kwa zaidi ya miezi miwili na nusu. Hii ni rekodi ya ajabu kwani mtu huyu alikuwa hawezi kukaa zaidi ya siku 10 nchini. Ikumbukwe mara tu alipochaguliwa kuwa Raisi alifanya safari za kujitambulisha katika mabara yote. Hicho kilikuwa ni kituko kwani hakuna kitu kama hicho katika masuala ya kibalozi na kiuraisi. Na hilo alilifanya baada ya kuwa Waziri wa Mambo ya Nje kwa miaka kumi! Baada ya hapo kila siku ya kumi alikuwa kiguu na njia na kufikia kutuambia kuwa anakwenda kuhemea na kuwa hawezi kubakia hapa kugawana umaskini.

Sasa ninajiuliza kuwa ikiwa atachaguliwa, kitu ambacho inaelekea hakiwezekani, je si atakuwa anafanya matanuzi ya nguvu na kuondoka nchini kila siku ya tatu? Hali hii imejitokeza nchini Zambia ambako gazeti la Post la Zambia liliandika makala nyingi kuhusiana na ziara zisizokwisha za Raisi huyo. mojawapo ni The Post Newspapers Zambia - Latest News, Politics, Business, Sports, Photos, Videos » Main Story » Rupiah is an absentee President

Hivyo basi kama Kikwete atarudi katika kitebe, kigoda au kiti cha uraisi ninapenda kuwaambia mjiandae kuwa na raisi msafiri huku mwanae akifanya anavyotaka.

Ewe Mwenyezi Mungu Iokoe Tanzania!
 
Ametambua wahisani siyo wanaompa ugali ila ni sisi ambao kila siku haachi kutuponda akidai bila ya misaada hakuna maendeleo ikimaanisha ya kuwa sisi hatuna uwezo wa kujiendeleza wenyewe.

Hata hizi kura sijui anazitafutia za nini kwa wale anaotunyanyapaa?
 
Sasa tufuate lipi?

Akitoka, ...huyo Vasco da Gama!

Akikaa nchini, ...huyo kavunja rekodi!
 
Kama ana kifua asafri sasahivi, mana akirudi nchi imeshachukuliwa!
 
hahahhaha
ulitakiwa kuweka msisitizo kuwa Amevunja rekodi yake mwenyewe. Ingekuwa kwenye mbio watangazaji nasikiaga wanasema "his own personal best record time"

Sababu nahakika hiyo rekodi marais waliomtangulia kwao sio rekodi .

Nadhni kupunguza matumizi na gharama JK alitakiwa awe rais na waziri wa mambo ya nchi za nje?
 
Sasa tufuate lipi?

Akitoka, ...huyo Vasco da Gama!

Akikaa nchini, ...huyo kavunja rekodi!
You are asking for the obvious my friend....I don't think you even deserve to login in on this forum for that matter!!
 

Labda tumuulize ni wangapi wamekufa njaa katika kipindi hiki ambacho hakutoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…