Kikwete awaalika wanamuziki wa kundi la Diamond na viongozi wao

mwa 4

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2013
Posts
3,390
Reaction score
751
Wasanii na viongozi wa WCB waalikwa nyumbani kwa rais mtaafu Jakaya Kikwete


Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete Jumatano hii aliwaalika wasanii wa label ya WCB pamoja na viongozi nyumbani kwake na kula nao chakula cha mchana.

JK ambaye ni mmoja kati ya marais ambaye amesupport sana wasanii wa muziki nchini, aliwaalika wasanii hao nyumbani kwake na kuzungumza nao mambo mbalimbali kuhusu muziki wao.

Mmoja kati ya viongozi wa juu wa label hiyo, Sallam alimshukuru rais huyo kwa kuwaalika nyumbani kwake na kuzungumza nao mawili matatu kuhusu muziki.

“Former President JM Kikwete and Former First Lady Mama Salma Kikwete. Asanteni kwa mwaliko wenu!! Allah awape afya njema,” Sallam aliandika instagram
 
safi sana my presidaa Mungu akupe maisha marefu, bado tunahitaji michango na mawazo yako katika kuendeleza Taifa hili
 
Nakumbuka Enzi za JK Said Fella akiwa anahojiwa aliwahi kusema "Tumempata rais anayependa michezo na burudani, wasanii tumtumie vizuri ipo siku tutapata rais anayependa fani tofauti tutakosa support"

Taratiiibu naanza kumuelewa Fella
 
Yaelekea bado support yake ipo kwenye tasnia ya mziki wa tz!
 
Aisee mheshimiwa nimeipenda sana hii kitu kweli wewe ni mtu wa watu aisee ninakutakia maisha marefu
 
Tunategemea single yake hivi karibuni nafikiri itaku atamshirikisha Hamonawizi
 
Safari hii Magogoni hakusomeki ni bora tu muende huko Msoga....baraka ni zilezile tu.
 
Mwisho wenu ni hukohuko msoga ikulu wanaingia wawekezaji tuu na watu na heshima zao kama mmeimiss sana iangalieni kwenye note ya elfu moja mlale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…