Kikwete bado apeta kwa umaarufu kuzidi wanasiasa wengine

Tatizo kwa sasa ni ninyi VIONGOZI. Hakuna mbadala wa JK kwa sasa. Jipangeni upya. Kule Uingereza Conservatives wamehangaika sana kumpata mbadala wa Tony Blair. Sasa wamempata Cameron na watachukua uongozi wa Nchi hata kama uchaguzi ungeitishwa leo!

Utafiti uliofanyika hauakisi hali halisi. Uongozi wa JK umekuwa mbovu mno katika historia ya Tanzania. Hakuna maamuzi kwa maslahi ya taifa-nchi yetu sasa ni kama gari linalotembea bila dereva.

Pia nakubaliana na waliosema kuwa ni vizuri kujua chanzo cha waliotoa tayarifa za utafiti ni watu gani hasa na walichaguliwa vipi kujumuishwa katika utafiti. Isije ikawa ni utafiti uliofamyika ukiwa na muelekeo wa kutoa majibu mazuri kwa JK.
 
bila methodology ya kueleweka hapa uzushi tu.

Kwa mfano, kama utafiti hau guarantee privacy, KJ anaweza hata kupata 100% popularity kwani Watanzania hawakawii kufikiri hawa pollsters ni mashushushu wanafuatilia nani mpinzani wamshughulikie.

Hiyo ni aspect moja tu.
 
Koh koh koh....MMhm!

Kama tafiti zenyewe ndio hivi kazi ipo Tanzania kuleta mageuzi ya dhati.Lakini kweli hii tafiti ina walakini kweli kweli kwa sababu inaacha maswali mengi kuliko majibu.Kwa uongozi wenyewe wa JK jinsi ulivyo loose namna hii tusubiri tuone.
 
Kwa kumlinganisha Kikwete na hao wengine wanaojiita viongozi wa upinzani ni wazi Kikwete atakuwa juu, kwani hawana lolote la maana. Lakini ukweli ni kwamba huyu bwana angekaa tu pembeni baada ya 2010. Kama kiu yake ilikuwa ni kuwa rais wa nchi hii basi tayari ameshaonja urais, inatosha! Hapa tunapaswa kujadili jinsi ya kumpata rais bora zaidi 2010. Kuongoza nchi si lelemama!
 
Utafiti si kitu chochote wakenya wafanye utafiti kujua kiongozi yuko popular kwenye nchi hii, sample wameisuka ili waendelee kupewa tafiti za serikali tunawajua janja yao wanachotaka ni consutancy work wakenya wa steadman hawana lao hakuna atakeyeheshimu utafiti wao wababishaji hao tafiti zao nyingio zimekataliwa kwenye mizania za wasomi
 
kikwete hawezi kuwa na umaarufu kiasi hicho kwa sasa.Wengi wape ila inawezekana wengi hao wakawa vichaa,Je bado utawapa? Naamini wamefanya utafiti kwa watu wa namna hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…