Jamani eeeh... kama alivyosema Mtanzania, tushukuru hizo polls zimeshuka kwa kiwango hicho...Siku zote tujiandae kwa habari mbaya kuliko njema na polls kama hizi ziwe kiamsho kwa wananchi kwamba vita yetu bado kabisa haijafikia ushindi..
Binafsi sipendi kabisa CCM irudi jukwaani lakini nafahamu fika Kikwete bado ana mvuto mkubwa sana kwa baadhi ya watu tofauti na wengi tunavyofikiria...Hiyo asilimia 62 imenipa moyo sana kwa sababu naamini kabisa kuwa wabunge wengi wa CCM walipita kutokana na nguvu ya Kikwete akiwa ndani ya Mtandao..NBa polls siku zote hupigwa toka mitaani na kwa idadi ndogo sana na watu.. Still, kati ya kila watu 10 haiwezekani wote mkafikiria sawa..
Sasa kama wananchi wameanza kuunganisha vitu hivi viwili tena wakati huu mbaya wa uchumi duniani nina hakika by 2010 rating ya Kikwete itakuwa chini zaidi..
Nina hakika wananchi hawataafiki sababu zozote zinazohusiana na hali ya Uchumi duniani kuwa ndio sababu bali Kikwete mwenyewe..Na laukama wapinzani wakijipanga na list ndogo tu ya Mbowe, Dr. Slaa, Lipumba na Mtu mwingine maarufu toka Zanzibar..Basi ushindi umepatikana..Kikwete can't stand alone kitaifa anaweza kushinda ndani ya CCM lakini Kitaifa itategemea na wapinzani wamejipanga vipi..
It's gonna be the Only time ya kula Turkey! -Thanksgiving day..[/QUOTEa]
Mkuu,
well said but only if wishes were horses everyone would ride one. Hata wewe leo hii ukiweza kupata pesa ya ufisadi ukawahonga NEC na CC ya sisiwehu utaukwaa urahisi bila hata kutumia sera kwenye kampeni bali ahadi kibao kama vile watu walale tu bila kufanya kazi na watapata maisha bora kwa kila mdanganyika. Uelewa wapiga kura ni karibu na hakuna.
Kuna wakati nilienda kwa babu yangu huko Sengerema nikakuta mzee mmoja pale kijijini ambaye kwa pale anaonekana ndio muelewa yuko kwenye foleni anasubiri mahindi ya mgao(msaada). Kukatokea ubishi wa kisiasa kuhusu rafu alizofanyiwa Masha na William Shija. Yule mzee mjuaji akaanza kuwasifia FFU kwa kumpiga Masha wakati inajulikana wazi kuwa masanduku yaliyokuwa yaamue hatima ya shija yalitoweka na hayakujumuishwa. Kwa baraka za msimamizi (mkurugenzi wa halmshauri) matokeo yakatangazwa Shija kashinda. Na hayo ni masanduku ya hapo Sengerema mjini ambapo shija alikuwa hatakiwi. Kwa ujumla Hata kama wapinzania wote wakiungana haki haiko upande wao. Wakazanie tu wabunge sehemu wanazokubalika.