Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
RAIS Jakaya Kikwete amesema Serikali haina mpango na kamwe haiwezi kuzuia kampuni ya kitanzania au Mtanzania kushiriki utafiti na uchimbaji mafuta na gesi ingawa ni gharama. Pia Rais
Kikwete amebainisha kuwa Serikali imeweka utaratibu wa kuhakikisha Watanzania bila kujali maeneo na wa kizazi cha sasa na kijacho, wananufaika na rasilimali zote asilia za nchi, kwa
kuhakikisha mapato yanayopatikana kutokana na rasilimali hizo yanafikia Watanzania wote.Alisema hayo wakati akizungumza katika kongamano lililoandaliwa jijini Dar es Salaam jana na viongozi wa
dini nchini, kuhusu rasilimali za gesi asilia, mafuta na madini kwa amani na maendeleo ya Tanzania.Kazi ya kutafuta gesi na mafuta si ya mchezo, inahitaji uwezo mkubwa kifedha na
kampuni nyingi zinazoomba fedha hapa ni zile zenye uwezo mkubwa kimtaji na zinazoaminika na benki duniani, kampuni ya Tanzania yenye uwezo huo mimi siijui, ingekuwapo wote tungeiona,
alisema Kikwete.Ugumu wa utafiti Rais alisema utafutaji gesi na mafuta, una gharama kubwa na hufanyika kama kamari ambapo uwezekano upo wa kupata au kukosa.Alifafanua kuwa utafutaji wa
mafuta na gesi, ulianza tangu wakati wa Ukoloni mwaka 1952 na kisima cha kwanza kilichimbwa mwaka 1956.Utafiti huo ulifanywa na kampuni za nje na uliendelea bila mafanikio nchi kavu na
baharini mpaka mwaka 2007, ambapo watafiti walihamia bahari kuu, kutokana na imani kuwa kuna uwezekano wa kupata mafuta au gesi.Katika bahari kuu, alisema, utafiti huo uliendelea mpaka
mwaka 2010 ndipo uvumbuzi mkubwa wa gesi ulipatikana na baada ya hapo visima zaidi vilivumbuliwa na mpaka sasa kwa uvumbuzi huo, Tanzania ina hifadhi ya gesi kiasi cha futi za
ujazo trilioni 46.5.Sasa Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye gesi nyingi duniani, alisema Rais Kikwete na kuongeza kuwa kuna kampuni inafanya utafiti Tanga, na imedai ina imani kuwa
itavumbua hifadhi kubwa ya mafuta kuliko ya gesi.Sasa matumaini ni makubwa. Akifafanua gharama za utafutaji gesi zinazotumiwa na kampuni hizo, Rais Kikwete alitoa mfano wa watafiti wa sasa ambao wamejenga jengo lenye ukubwa sawa na Hoteli ya Kilimanjaro Hyatt ya Dar es
Salaam katika bahari kuu.Mbali na ujenzi huo, alisema wawekezaji hao wanatumia mashine ya kuchimba ambayo huingia ndani ya bahari kwa kina cha kilometa mbili mpaka tatu, ndipo wakute
ardhi na baada ya hapo huchimba kilometa zingine mbili au tatu, kuikuta gesi.Kwa siku, mashine hiyo inagharimu dola za Marekani milioni moja (zaidi ya Sh bilioni 1.63) kwa siku, alisema Rais
Kikwete na kufafanua kuwa mpaka kuvumbuliwa kwa rasilimali hiyo, visima zaidi ya 40 vilichimbwa na kukutwa bila kitu.Kipaumbele cha serikali Rais alisema katika utafutaji gesi na mafuta gharama
ni kubwa, mbali na mashine yenyewe ya kuchimba kugharimu zaidi ya dola milioni moja kwa siku, bado uwezekano wa kuvumbua ni mdogo na ni kama kamari.Kutokana na asili ya utafiti ilivyo, Rais
Kikwete alisema hawezi kuchukua fedha za Serikali na kuziingiza katika utafiti wa aina hiyo, wakati anatakiwa kutoa huduma kwa Watanzania, ikiwamo afya, elimu, miundombinu na
nyingine.Manufaa, wazawa Kutokana na hali hiyo, Rais Kikwete alifafanua kuwa Serikali iliunda Sera ya Gesi na Sheria mpya inatarajiwa kutengenezwa na msingi wa sera na sheria hiyo,
uchimbaji ukianza, mapato Serikali itapata asilimia 70 au 65 na mwekezaji asilimia 30 mpaka 35.Mwekezaji atumie gharama zake kutafuta, akikosa hatuna hasara, akipata tunakaa kujadili
gharama zake ndipo aanze uchimbaji huku akitoa gharama zake kidogo kidogo, akimaliza mgawo wa mapato asilimia 70 ya Serikali, asilimia 30 yake kuna ubaya gani? Alihoji Rais Kikwete.Mapato
hayo kwa mujibu wa Rais Kikwete, pamoja na mambo mengine, yatatumika kuwezesha Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) nalo liingie katika utafutaji gesi na mafuta. Na wao wakipata gesi,
baada ya kutoa gharama zao kidogo kidogo, tutaanza kugawana mapato asilimia 30 zitakwenda TPDC, asilimia 70 serikalini, alisisitiza.Kwa sasa TPDC, wamekuwa wakitoa zabuni tu na kutoa
leseni za utafutaji gesi na mafuta. Rais alisema baadaye, Serikali itauza hisa zake za TPDC kwa Watanzania kama ilivyofanyika kwa benki ya NMB na mashirika mengine ya umma ambayo Serikali
iliuza hisa zake.TPDC pia kwa mujibu wa Rais, inaweza kuuza hisa kwa kampuni za kitanzania, lakini hata baada ya kuuza, bado mapato ya gesi asilimia 70 yatabaki ya Serikali na asilimia 30 ya
TPDC na wabia wake.Hii asilimia 65 hadi 70 ni muhimu kubaki serikalini, katu hatuwezi kuiachia kampuni mgawo wote, hata kama ni ya kitanzania, ikumbukwe kuwa fedha zitakazopatikana
kutokana na nishati hizi zitatumiwa na Serikali kwa manufaa ya Watanzania wote na si Kikwete na wanawe, itakuwa Serikali na wanawe ambao ndio Watanzania, alisisitiza. http://www.touch.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/20961-kikwete-hatuzuii-watanzania-kuchimba-gesi