Kikwete hulipwa appearance fee?

Sasa ndio nimeshafahamu kwa nini Dr. Shein anatembea na mkasi mfukoni!!!

(Just kidding!)
 
Sasa, huu utaratibu unaongozwa na sheria yoyote? hiyo kampuni ya wakala wa wabunge imeingia mkataba na Bunge au na Spika? Ilipatikana vipi? Je hawa wanaoandaa hizo za Rais wanafanya hivyo na kulipwa na nani? Ni rate gani kwa kufungua shule ya binafsi, kuzungumza kwenye warsha fulani binafsi n.k? Kama watu hawataki kulipa Rais haji?
 
Wanaita Honoraria something like that. Ambayo waheshimiwa hupata hata akienda kwenye kikao akaongea pumba na kuondoka who cares!!
 
Naomba ni changie kipengele cha Fina, Anachokifanya huyu dada kinaitwa lobbying ambayo ni branch ya PR.

Kwa nchi zilizoendelea lobbying inalipa zaidi ya PR lakini mara nyingi malobbyst wanaishia katika kashfa na rushwa, ila si lazima but that is one of the risk.

Sasa kama kampuni au mfanyabiashara anataka hiyo huduma na hajuai wapi pa kuanzia akienda kwa fina anapatiwa huduma kwa makubaliano maalumu. Serikali inanufaika kwa upande wa kodi kutoka kwa fina na hao wanaohitaji huduma kwa namna moja au nyingine.

Kwa upande wangu nampongeza Fina kwa kujiajiri katika hii branch ambayo pale nyumbani si maarufu sana.
 
mkiambia standards za JF zimeshuka manaanza kulalama

kwanza nilitegemea mngeanza kumkoma nyani GILADI kwa kuleta jina la hiyo PR FIRM na iko owned na akina nani na kazi gazi imeshafanya na kiasi gani inatoza

then mtaanza kuuuliza maswali mengine

Hivi mnakumbuka enzi zile JF ilikuwa maarufu kwa kuwa na data na docs?

Imagine hii listi ya matumizi ya wabunge leo SLAA anayo sisi hatuna...i dont know where we kept out eye off the ball

Tazama issue ya DECI hivi mpaka leo the so called wachambuzi wetu wameshindwa kuleta majina ya ma Stake holders wa DECI sasa matokeo yake tunaongea kama wale jamaa waonao jibizana kwenye print media yetu ambayo at most imejaa majungu na copy and paste journalists
 
Mkuu mwanakijiji, hii inayojishughulisha na Mkulu siijui,ila kuna ile ya Mdada Fina Mango,ili ufanye hafla/presentation kwa wabunge lazima upitiye kwake,anabaraka zote za spika na wabunge wetu wanalijua hilo!!

Bongo bana ulaji nje nje huyu dada sasa anakula bata tu.....kha! kufa kufaaana mapande tu kila kona.
 
I hope hatutakuja kuambiwa mkulu analipwa sitting allowance ya vikao vyake ikulu... Maana mh...
 

Mzee Mwanakijiji!

Kwa uzoefu nilio nao a sitting head of state hawezi kulipwa ""any appearance fee"" what ever you like to call it! Kwanza JMK for all the years almost twenty sijaona akiwasilisha paper apart from kuhudhuria netball na mpira wakimlipa huo ni usanii tu!

Marais na Mawaziri wakuu wa zamani huwa wanalipwa tena good money kwa kutoa mada that is ni kule kwa wenzetu! Very few people apart from CCM wanaweza kupokea mihadhara from condemened criminals like BWM japokuwa mwenyewe akili zipo ila alipofiushwa na rushwa! Hilo la Kikwete time will tell tungojee amalize ngwe zake !Akiwa madarakani tabu kujenga hoja si tuliona ule mdahalo wa IMF alivyotuaibisha je akiwa mstaafu si ni kasheshe mgosi!! na KWA MWENDO anaokwenda na mafisadi sijui kama ataweza hata kutembea kule Chalinze na Mboga bila heavy ammunition!!
Kikwete unataka kutuachia legacy gani??? Learn from your mentor Nyerere or go South and talk to Nelson Mandela !!!Babu lakini mpaka leo Dunia inamheshimu kichizi!!!! Mzee Mwanakikiji mwambiee!!!!
 

Anza na mtoa mada, inabidi uchambuzi makini ufanyike, sidhani na siamini kama kitu hiki kipo especially kwa Rais anapokuwa anafanya kazi za humu ndani. kama ni appearance ya wabunge na viongozi wengine kwa shughuli ambazo sio za jamii say za biashara kwanini tusiwalipe? appearance yao kwetu ni biashara so WHY NOT PAYING THEM, I REPEAT SIPENDI KUAMINI KUWA WANALIPWA KWENYE SHUGHULI ZA KIJAMII ZAIDI.

Hiyo PR ya Mango Fina ni si ni ya kibiashara????

Kwa Bongo inawezekana kwani hata akina naniii ukiwaita waje kwenye hafla yako waweze kuripoti kwa umma, bila BROWN ENVELOP huwaoni ng'o!!!!!!
 

Kile unachokisema kimesababisha JF standard kushuka ndicho unachokifanya; kulalama. Kama unaona jambo haliendi lilivyo au linapaswa kufanywa tofauti, onesha njia usitegemee "wachambuzi" wakulimie, wakupandie, wakuvunie na kukutafunia.

Swali lililoulizwa kama hujalielewa ndilo linaita hivyo unavyoviuliza.. kwamba ni mlolongo wa maswali, maswali ambayo yakipatiwa majibu basi tutakuwa tunaelekea kupata data tunazozitafuta. KUmbuka, kuuliza maswali ni sehemu ya kutafuta data! Haiwezekani umkome nyani giledi bila kuwa na msingi.

Kuhusu Dr. Slaa kuwa na docs fulani wakati "sisi" hatuna, inashangaza unategemea mtu mwingine atafute wakati na wewe ni member mkubwa tu hapa JF, Dr. Slaa si yumo humu ungeweza kumpm au kumpigia simu. Unatarajia nani afanye hilo?

Kile unachoweza kufanya usisubiri mwingine afanye na asipofanya usilalamike kwani na wewe unauwezo wa kufanya. Hiyo inaitwa hekima, na wengine wanaita kujituma.
 

Ndiyo maana yanaulizwa maswali "kudhani" kuwa kitu hiki hakifanyiki haina maana hakifanyiki. Wengine hata tulikuwa hatujui kuna kampuni ya PR inayofanya kazi na wabunge na inakusanya mapato! Kama hupendi kuamini ni uamuzi tu kwani mtu anaweza akakataa dawa si kwa sababu ya kisayansi bali kwa sababu haamini kuwa inaweza kumponya!
 

nilikuwa namuonea fina huruma baada ya kumwagwa craaaaus FM!!! kumbe bado anakula bata! swafii tuu!
 
Kuhusu sitting allowance aka appearance fees, viongozo wote wa sirikali wanavuta. Ila kinachosikitisha ni kwamba wabunge huwa wanavuta more than once for the same meeting/warsha. e.g kamati ya kudumu ya bunge inaweza kwenda kutembelea agency fulani alafu hiyo agency ikawalipa sitting allowance at the same time hao wabunge wanakuwa wamelipwa na bunge sitting allowance ya kikao hicho hicho. Ndo maana nakumbuka waziri *** alikuwa akisafiri analipwa na wizara husika posho ya safari na kila ofisi atakayotembelea mkoa husika anagongwa na posho nyingine tena. Hili lina fanyika mpaka kesho. Na ndio maana bongo UBUNGE ni boooooonge la dili. Sasa hivi nasikia tetesi kuna jamaa wanachangisha pesa ili wamng'oe mbunge fulani machachali mkoa wa Rukwa!!

Siasa ni bonge la carrier bongo kiliko fani nyingine yoyote ile wana JF
 
GameTheory,
Mkuu maneno yako kweli kabisa. navyoifahamu JF enzi zake hii hoja ya Mwanakijiji ingejibiwa haraka sana na data zaidi kutolewa lakini siku hizi habari nyingi zinatoka magazetini.. Kila kinachoandikwa magazetini ndicho kinachokuja hapa kujadiliwa, tena mara nyingi ukisoma magazeti yenyewe utaona kuna maoni ya watu wengine huvutwa tena hapa..Yaani tumeishiwa muflisi na kitu kimoja kikubwa ni kwamba wakali wengi wa JF wamejimegua siwaoni tena..
Vipi Nyani Ngabu katinga Bongo hana mtandao nini!... maanake simsikii kabisa kulikoni, sii kawaida!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…