Kikwete kupata mlo wa mchana na wasanii wa bongo flava leo dodoma

Kikwete kupata mlo wa mchana na wasanii wa bongo flava leo dodoma

tikotiko

Member
Joined
Jul 9, 2010
Posts
26
Reaction score
0
Baada ya wasanii wa bongo flava kumsifia sana JK na CCM yake kwenye kikao kilichomalizika juzi mkuu wa kaya ameamua kuwaita na kupata nao chakula cha mchana leo!!
Itakumbukwa baadhi ya wasanii wanajulikana ka staili yao ya mavazi na kujihusisha kwao na vitendo visivyofaa (si mnakumbuka TMK?? na skendo zake??) basi hawa jamaaa leo wanakula mlo wa mchana na mheshimiwa sana!!
Nawakumbusha tu; kwenye kikao kilichomalizika juzi Mzee Mkapa, Karume na Mzee Ruksa hawakuonekana kushabikia hawa wasanii hata kidogo...hasa BM, alikuwa ame-fume ile mbaya, tofauti na JK ambaye alikuwa anatabasamu muda wote...hasa kila jina lake linapotajwa!!
Kwa wale tuliopo Dodom akwa sasa nadhani tunaweza kukaribia pia.....
Haya mlo mwema!!!
 
Mkuu, wakati wa campaign tegemea kila kitu... hata rais kuvaa mlegezo na kofia kubwa na eye patch kama "kalapina"... usishangae ukaona ameweka dawa kama banana zorro na kupiga cheni kali kama sugu... NDIO MAANA YA KAMPENI

Zikishaisha ndio masuala nyeti yanarudi...
 
Hao wasanii wa Tanzania kweli vipofu
 
Baada ya wasanii wa bongo flava kumsifia sana JK na CCM yake kwenye kikao kilichomalizika juzi mkuu wa kaya ameamua kuwaita na kupata nao chakula cha mchana leo!!
Itakumbukwa baadhi ya wasanii wanajulikana ka staili yao ya mavazi na kujihusisha kwao na vitendo visivyofaa (si mnakumbuka TMK?? na skendo zake??) basi hawa jamaaa leo wanakula mlo wa mchana na mheshimiwa sana!!
Nawakumbusha tu; kwenye kikao kilichomalizika juzi Mzee Mkapa, Karume na Mzee Ruksa hawakuonekana kushabikia hawa wasanii hata kidogo...hasa BM, alikuwa ame-fume ile mbaya, tofauti na JK ambaye alikuwa anatabasamu muda wote...hasa kila jina lake linapotajwa!!
Kwa wale tuliopo Dodom akwa sasa nadhani tunaweza kukaribia pia.....
Haya mlo mwema!!!

Sijaipenda signature yako mkuu! Unaturudisha nyuma, dont play with this matter
 
Hao wasanii wa Tanzania kweli vipofu

Siyo tu vipofu mkuu, hiyo ni kuendekeza njaa na nawashangaa sana sana wale wanakwaya wa injili!!
Wale wa Bongo flava pamoja na Vicky wao tunajua ni kwanini walikuwa pale, ila wale wa injili duu kweli 2010 tutaona mengi.

Hapo kwenye red mkuu uko sahihi ila ni kuendekeza njaa pia.
 
siwashangai sana wasanii japokuwa kuna baadhi yao sikuwategea.wanaganga njaa.ngoja uchaguzi upite na mkwere achukue nchi tena Flora Mbasha huyo kusoma masters nje (na hana hata certificate) kaaaaazi kweli kweli
 
Oya huyo mkwere alishapinda long time ago kwa hiyo sishangazwi na maamuzi yake. Alipaswa kufanya shughuli nyingi za kijamii kama vile kutembelea ofisi za serikali hapo dom ajionee wafanyakazi wake wanavyo taabika,sekondari na kadhalika yeye anajali wasanii ambao wengine wameingia kwenye muziki kibahati.
 
Njaa, asante kwa ushauri, naheshimu maoni yako!! Tuko pamoja
 
Kwa kipindi hiki cha campaign jamaa atafanya kila liwekanalo kupata ushindi, hata kama akiona kucheza na kichaa kutamlipa yeye kurudi magogoni I bet jamaa ataafiki tu! kwa wasanii wa muziki hapo sina la kusema! si mnamkumbuka Mr Ebbo aliimba " umezoea kiti moto eeeeh, njaa inaumwa, angalia usichinje nyau! bongo flava njaa inawauma sasa wanachinja nyau!
 
Back
Top Bottom