Mojawapo ya mabango ya kampeni za ccm, linamwonyesha JK akinong'onezwa jambo na mzee mmoja, likiwa na ujumbe
"JK ANAWAJALI SANA WAZEE".
Picha hizi zinaonyesha jinsi JK anavyowajali wazee.
Wazee wastaafu wa jumuiya ya Afrika ya mashariki wakiwa nje ya lango kuu la kuingilia ikulu, wakitegemea Rais Kikwete angewajali ili awasaidie walipwe mafao yao, lakini waliondolewa kwa virungu vya polisi
Hapa siyo uani mwa nyumba ya mtu, la hasha, hapa ndiyo makazi ya wastaafu wa jumuia ya afrika ya mashariki nje ya ofisi za makao makuu ya shirika la reli kando kando ya barabara ya UHURU, wameishi hapo kwa zaidi ya miaka mitatu.
Baada ya juhudi zao za kudai haki yao kugonga mwamba mgumu wa serikali ya chama cha mapinduzi, wastaafu waliamua kufunga barabara ya H.Mwinyi eneo la daraja la selender. Waliondolewa kwa nguvu za jeshi la polisi
MAMA alishindwa kujizuia jinsi ZULUMA inavyozuia mafao yao. Analia kwa uchungu mkubwa akijigaragaza barabarani.
Vikongwe wa Afrika ya mashariki wakila mkong'oto kutoka kwa askari polisi kuwaondoa barabarani
Serikali ya JK ilitumia kila aina ya zana kuhakikisha hawa wazee wanazibitiwa. Hapa ni nje ya ofisi za shirika la reli.