mzeewabusara
Member
- Jun 7, 2006
- 12
- 24
Wakati Mheshimiwa Mkapa anamaliza uongozi wake alikiri kuwa eneo mojawapo ambalo halikupewa umuhimu katika uongozi wake ni KILIMO. Kutokana na jinsi Mheshimiwa Raisi Kikwete alivyoanza katika kasi yake bado sijaona kama kweli suala la kilimo limo sana katika ajenda. Hivyo napenda kutoa ushauri ufuatao.
1. Mabadiliko makubwa ya uongozi wa wizara ya kilimo yanatakiwa ili kupata viongozi watakaoweza kubuni na kuanzisha mikakati mipya ya kilimo. Nasikia waziri aliyepo sasa hakufanya vizuri katika wizara ya elimu aliyoongoza kabla ya hii. Kama ni hivyo Mheshimiwa Kikwete ni vema ukaliona hili na kufanya mabadiliko mapema.
2. Wizara ya kilimo iandae sera na mikakati ya umwagiliaji wa maji
3. Wizara ikaribishe wawekezaji wakubwa wa kilimo kama wale waliokuwa wakilima Zimbabwe na tuwatie moyo matajiri wa Tanzania kuwekeza katika kilimo.
4. Serikali ianzishe programme ambazo zitahamasisha vijana kupenda kilimo badala ya kuuza karanga na korosho pale chalinze. Hii inawezekana mfano kwa kuwa na mashamba makubwa ambayo yataajiri vijana kwa kazi mbalimbali za kilimo. Hii inawezekana .
5. Mwisho Tanzania kama tunataka kupiga hatua at least ya kuhakikisha tuna chakula chetu wenyewe suala la kilimo NI MUHIMU SANA. Mtazamo wangu hadi sasa naona serikali bado haijaupa mkazo kilimo.
Wana bodi naomba tujadili na kutoa mawazo yetu ili nchi yetu yenye mito maziwa isiwe tena ni nchi ya njaa na ombaomba. Inatia aibu jamani.