BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Christopher Nyenyembe, Mbeya
Tanzania Daima~Sauti ya Watu
WAFANYAKAZI waliopunguzwa kazi katika mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira (KCM), mkoani hapa mwaka 2005, wanaoidai serikali zaidi ya sh bilioni 47, wamemgeuzia kibao Rais Jakaya Kikwete, wakimtaka aongozane na maofisa wa hazina watakaowalipa fedha hizo.
Hatua hiyo inayoonekana kumtega Rais Kikwete, imetokana na taarifa kuwa Rais Kikwete, anatarajia kufanya ziara yake ya kwanza katika mkoa huu hivi karibuni.
Baadhi ya wafanyakazi waliozungumza na Tanzania Daima, jana walisema wanataka kuonana na Rais Kikwete ili wamfikishie kilio chao ambacho hakijapatiwa ufumbuzi tangu walipopunguzwa kazi.
Wafanyakazi hao walidai kusikitishwa na hali hiyo, kwani hata kamati ya rais aliyoiunda kuchunguza sekta ya madini na mikataba, ilipita katika mgodi huo na kupokea kilio cha wafanyakazi hao, lakini bado hawajalipwa fedha zao.
Wafanyakazi hao wanaililia serikali kwamba hawajalipwa mafao na mishahara yao ya miezi kadhaa waliyokuwa wakidai tangu mgodi huo ulipokuwa chini ya serikali na kuwafanya washindwe kuondoka kwenye nyumba za mmiliki mpya aliyekabidhiwa mgodi huo.
"Baada ya suala letu kushindikana kwa muda mrefu, sasa tunataka kutumia ujio wa rais kuwasilisha kilio chetu kwake kwani ndiye pekee aliyebaki kutusaidia," alisema mmoja wa wafanyakazi hao.
Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Migodini (TAMICO), Thomas Cheyo, alisema jana kuwa hali za wafanyakazi hao waliopunguzwa kazi tangu mwaka 2005 ni mbaya na wengi hawana chakula, hivyo ujio wa Rais Kikwete ni faraja kwao.
"Tumepata taarifa kuwa Rais Kikwete anakuja Mbeya, tunaomba atembelee hapa mgodini ili tuweze kumfikishia kilio chetu, tangu tulipopunguzwa kazi mwaka 2005, tunaidai serikali mafao yetu ya zaidi ya sh milioni 47 lakini hatujalipwa, wengine wamekufa, wengine wana hali mbaya, hata Mbunge wetu, Dk. Harrison Mwakyembe tumemueleza," alisema Cheyo.
Alisema kitendo cha serikali kushindwa kuwalipa haki zao, kimewazidishia ugumu wa maisha na hawaelewi yupi mwenye jibu sahihi kuhusu hatima ya malipo hayo.
Mkuu wa mkoa huo, John Mwakipesile alipohojiwa kuhusu nafasi ya rais kuutembelea mgodi huo katika ziara yake ya kikazi, alisema hajapangiwa kuutembelea mgodi huo.
"Rais kweli anakuja Mbeya, lakini hana ratiba ya kutembelea mgodi wa Kiwira katika ziara yake, kesho nina kikao na waandishi wa habari saa nane ofisini kwangu ili kuzungumzia ziara hiyo," alisema Mwakipesile alipokuwa akizungumza jana kwa simu.
Uamuzi wa serikali ya mkoa kutompangia ziara rais kuutembelea mgodi huo, kunaweza kuzidisha kilio cha muda mrefu kwa wafanyakazi hao ambao mkuu wa mkoa huo, Mwakipesile aliyewahi kuwa mbunge wa Jimbo la Kyela na kwenye bodi ya Kiwira, ni miongoni mwa viongozi wanaojua undani wa matatizo ya wafanyakazi hao, ambayo hayajapatiwa ufumbuzi.