Mzee Mwanakijiji,
Hii habari kama ni kweli si Dr. Mwakyembe aende kuwatetea na kuwatoa hao vijana? Kama mbunge ana wajibu wa kulinda maslahi ya wapiga kura wake.
Ungewashauri waliokutumia ujumbe waufikishe pia kwa mbunge wao ili kama hana habari basi achukue hatua.
Itakuwa ni ukichaa kuwakamata vijana kwasababu tu wanalalamikia uongozi uliopo.
Huyu Mwakipesile anajifanya mungu mtu?. Wananchi wa mkoa wa mbeya hawakutaki kwanini wasiseme?. Mwakipesile na kundi lake waachilieni vijana hao mara moja ama na wewe watoto wako hawatakwenda shule ama popote pale.
Sasa naelewa kwa nini JKN alikuwa hachagui mtu wa Mara kuwa kiongozi wa mkoa wa Mara. Haya matatizo yangeepushwa Mbeya.
Kwani Mwakipesile ilikuwaje akaupata Ukuu wa Mkoa?
mara wezi wa EPA wamepewa siku 72, mara mitihani kuvuja kuliko kawaida,Sishabikii fujo wala vurugu, ila nasema ................
............. "NA BADO!!"
Watu wameshachoka, wanaona viongozi hawashughulikii matatizo yao, kutwa kuchwa kupiga politiki na kufanya ziara tu, mara leo Mbeya kesho Marekani keshokutwa Mexico wakati nchi ina matatizo yanayohitaji kupatiwa solution.
Duh nimesikia tena wameupiga mawe msafara wa JK huko Chunya kijiji kimoja sikumbuki magari sita yameharibika mawili ya mawaziri...kazi kweli wanayo.
Kwa nini msafara wasafiri usiku?Halafu wanadanganya waliotupa mawe eti ni walevi,
Maana nasikia hadi gari la Salma Kikwete limevunjwa kioo na baadhi ya waandishi wamejeruhiwa