Kikwete Mbeya: Mgongano na wananchi na mwitikio wa serikali

...kitendo cha kurusha mawe kuelekea popote aliko rais ...hata kama haYAjampata its amount to trEason......unafikiri hao watu wakipatikana si watafunguliwa kesi ya uhaini.........wanasheria mnasemaje!!??

..nasikia kijiji kizima usiku mzima wanapata kipigo....hakia mungu!
 


Kuwapiga watu, wajue wana mwagia petrol kwenye moto, na wajiandae basi kupiga mamilioni ya watanzaia tulio choka!
 
Waandishi wa habari na wapiga picha si waende kwenye hicho kijiji jamani?

Waandish wa magazeti ya Mwananchi,Mtazania Daima anagalao hawatanunulika na jk waende huko ili watangaze na kuonyesha live.Nadhani huo mgogoro utakua maarufu sana na utachochea zaidi hasira ya watanzania dhidi ya serikali hii dhalimu.Nakwambia Jk atakua rais wa ikulu tu hatathubutu kufika mahali popote tena.


Kupiga raia kwa sababu gani,huu ni unyanyasaji.yaani aendelee kunyanyasa wananchi kwa kuwalinda wezi wa fedha zao na wananchi wakipaaza sauti anawapelekea polisi,yaani hata ambao hawakumzomea? Enough is enough. STEP DOWN MR. PRESIDENT!
 

Mungu nusuru taifa lako, hivi jamani huyu si ndiye tuliambiwa ni chaguo la Mungu? am confused je angekuwa ni chaguo la shetani hali ingekuwaje? pamoja na yote hayo yanayotokea kwa Muungwana na chama chake atarudi tena kwa wananchi hao hao kuomba ridhaaa? Hatujawahi kuwa na Kiongozi hopeless kama JK, sijawahi piga kura this time nitajiandikisha na kurudi bongo kutumia haki yangu ya kidemocrasia...my vote I am sure will make a difference...
 
[/SIZE]

Kuwapiga watu, wajue wana mwagia petrol kwenye moto, na wajiandae basi kupiga mamilioni ya watanzaia tulio choka!


Hata walimu wangu wamechoka na kulia machozi kwa sababu ya haki yao.

Huu ni utawala wa Shetani, huruma hawana kabisa.


Mawapa hongera sana wananchi wa Mbeya kwa kumuwajibisha,that's a very clear message.

MR.PRESIDENT,STEP DOWN
 


Mkuu wangu,

Heshima mbele sana,

Waliomtabiria kuwa Chaguo la Mungu ni wale manabii wa Baali,ili anguko la Baali (CCM) litimie kwani Mungu sasa anawatumia akina-Elia (Wananchi waliopigika,walimu waliogoma,wananchi wa Tarime,vyama vya wafanyakazi,wanafunzi walionyimwa mikopo wa UDSM na UCLASS etc) ili kufanikisha anguko la Baali
 
jamani,mie nimeitafuta hii habari nimeikosa,sasa mwenye habari za kutosha tafadhali aziweke humu,au aiskani hio stori ya nipashe atuwekee humu fasta ili tuweze kutoa fair comments.
 


Suala la msafara wa rais kupigwa mawe hata kama hakuumia hata mtu mmoja,suala tuu la kupigwa mawe linatosha kumaanisha kitu.
 

A ngeenda tu PERU akapumzike kwanza
 
Jana usiku kuna wananchi wa chunya wameletwa Hospital ya Rufaa Mbeya baada ya kupigwa na polisi walipovamia msafara wa Jk kwa mawe. Muungwana amekatisha ziara ghafra alikuwa anaelekea Mbozi akitokea chunya, Nitawaletea habari zaidi

Haya ni ya kweli lakini ama ndiyo habari za redio mbao?. Ni vyema kama tungepewa source za hizi habari.
 
Quote:
Originally Posted by single D

Kwa nini msafara wasafiri usiku?Halafu wanadanganya waliotupa mawe eti ni walevi,
Maana nasikia hadi gari la Salma Kikwete limevunjwa kioo na baadhi ya waandishi wamejeruhiwa
Samahani wana JF marekebisho kidogo nimefuatilia zaidi, walio umizwa ni watu wliokuwa kwenye msafara na waandishi na Salma amekoswa koswa gali lake limejeruhiwa


NADHANI HAPA KUNA WALAKINI WA HABARI NZIMA,NADHANI MTOA MAADA ANGEELEZA AMA KULETA HIYO HABARI KUTOKA KWENYE HILO GAZETI
 




Mkuu naona hutaki amini, tafadhali usitake kubadili mada, sio lazima uchangie move on with other stuffs.... wananchi wameamua kujichukulia sheria mikononi kujilaumu kwanini walimpa kura 2005
 
Sanda HIYO HABARI HAIJA TOKANA NA GAZETI MIMI NIPO HAPA HOSPITAL YA RUFAA MBEYA MAJERUHI WAMELETWA USIKU WA SAA TATU HIVI NA WALIOELEZEA KUHUSU TUKIO HILI NI ASKARI AMBAO WALIKUWA KWENYE MSAFARA NA NDIO WALIO LETA majeruhi NDIPO MMOJA WA ASKARI ALIPO ULIZWA NA WATU BAADA YA KUONA MAGARI MENGI YA POLISI ENEO LA HOSIPITALI AKASEMA MSAFARA WA RAISI UMEVAMIWA KWA MAWE NA ILIKUWA AENDE KULALA MBOZI AKAAHIRISHA AMELALA MJINI MBEYA SISI HAPA HOSIPITAL TUMESHUHUDI WALIO UMIA
 


Asante mwanangurumo kutupa za jikoni, hata hivo we Sanda kama uko bongo katafute nipashe wameandika na redio zote bongo leo zinazo chambua magazeti na kupokea maoni kwa njia ya meseji, leo ndo hii ilikuwa hot!

Kilicho nishangaza ni jinsi wengi wetu walivo furahia habari hii wakakandamiza kwamba labda kwa njia hii JK atavua hiyo miwani yake ya mbao!
 
Wagombea urais marekani wenyewe wana thamini elimu kwa kuweka kipaumbele kwanza kuboresha elimu yao na pia kuwaongezea mishahara walimu pamoja na kuwawekea mazingira mazuri ya kujiendeleza kielimu

Sasa leo nchi yetu hii changa kuwafumbia macho walimu na swala zima la elimu kweli tutafika? hujamaliza huko kuna wazee wetu kabisa wastaafu wa EA wanadai mafao yaho ivi hapo kweli hata kama baraka zinaombwa wazee hawa watatoa kweli?!!!

Kwaio moto huwa una anza kidogokidogo,mana mambo ndio yanavo anzaga ivivi mara watu wanachapana kimzaa mzaa,mana ndio tumesha anza ona mara Tarime leo Mbeya sasa sijui 2010 itakuaje!!!!

Nafikiri viongozi wetu wana akili timamu na hata wanao taka kuingia huko kwenye uongozi lazima wajifunze na chokochoko izi na kutatua kero.

AMANI IWE NANYI
 
..hii habari imeandikwa kwenye nipashe ya leo..na ni bahati imetoka kwani magazeti mengine yameogopaa kuitoa au yameombwa....hata hilo nipashe lenyewe kuna uwezekano mkubwa lisifike mikoani maana mtandao wananunua kopi zote ambazo zilikuwa hazijafika distribution....

ukitazama kwenye mtandao wa ipp bado haijawa uploaded na si kawaida ...ila ukifanya refine serch utaona hivi......
bonyeza hapo chini;

http://www.ippmedia.com/ipp/nipashe/2008/10/16/124601.html
 
Ni matokeo ya kulelewa hivyo, kama boss wao JAKAYA KIKWETE hayuko serious kwanini kwa kupesile asitumie mwanya huo???

Huko Mbeya kuna mambo. Akiwa Mbeya, JK aliwaweka wafadhili na wanasiasa katika ukumbi wa mikutano bila kutokea, katika hafla ya kuchangia fedha. Walikuwapo wabunge na baadhi ya wawakilishi wa kampuni mbalimbali.

Lakini jambo moja dhahiri ni kwamba, Mwakipesile ni matundan ya JK mwenyewe na yeye ndiye aliyempeleka huko, kwa hiyo hana ubavu wa kumdhibiti.
 
Huko tunakoelekea hakutabiriki. Mambo tusiyoyawazia yanatokea. Yaliyofikirika tu sasa ni dhahiri na inaonekana yatakuja mengi zaidi. Cha kujiuliza ni mkondo asilia ama kuna kutia viungo supu ichemke zaidi. Na kama ni hivyo huyo ni nani na kawekwa na nani kutengeneza cha nani kwa ajili ya nani? Tusameheane, huu ni mtazamo tofauti tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…