Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 239
Mwaka 2005 alipata 84%. Zimekwenda wapi hizo zingine? Lakini nakubali atashinda bcoz ours is a unique country -- sheep for humans!
Hivi kwanini REDET hawajawauliza wana CCM na Watanzania kama wanataka Kikwete awe mfalme na wawaone watu wangapi wataunga mkono wazo hilo!!
hIVI HUWA WANAPITA KWA KINA NANI NA KUFANYA TAKWIMU ZAO ZA UONGO ??
Sina uhakika kama walifika na kufanya interviews zako Kigoma, Tarime, Musoma, Buzwagi, Busanda, Moshi, Karatu, Dar na Pemba. Research inayofanyika bila uwazi inakuwa na utata sana - anyway wacha wakipe moyo chama chao.
Wadau nimedokezwa na Mdau mmoja hapa kwamba REDET ni ya Prof. Mukandala wa UD na kabla ya JK kuwa Presidaa, Mukandala aliahidiwa ukuu wa Chuo na JK. So Prof. Mukandala analipa fadhila kwa kampeni za chini chini na takwimu mbofu mbofu.
Jamani hebu nisaidieni kutoka asilimia 67.4 Oktoba 2009 hadi asilimia 49.3 March 2010 ni kupanda au kushuka kwa utendaji kazi wa Kikwete.Takwimu hizi zikilinganishwa na tafiti zilizopita za Redet inaonekana kiwango cha kuridhika na utendaji kazi wa Rais Kikwete miongoni mwa wananchi kimeanza kupanda. Oktoba 2009 ilikuwa asilimia 67.4, Oktoba 2007 ilikuwa asilimia 44.4, Novemba 2008 ilikuwa asilimia 39.5 na Machi 2010 ilikuwa asilimia 49.3.
Ni kweli Kikwete atashinda lakini sio kwa kishindo kama ilivyokuwa 2005..
hata huo ushindi nina wasi wasi nao, anaweza hata asishinde, kwani yeye nani jamani
utafiti wa redet huwa ni wa kwenye dawati tu hakuna field work
#27 masanja 2010-04-28
Hii taasisi nilifanyapo kazi ya ukibarua kwa muda wa miezi sita mwaka 2005. Imejaa wanamtandao, na uccm kwa kupita kiasi. data zilikuwa zinapikwa ili kufanikisha malengo fulani.
Hata haya matokeo siku zote najua yanapikwa ilikufanikisha mpango fulani. kwanza huwezi kuchoma pesa kutembelea majimbo 50 ukaja na wahojiwa 2500.
Uwezekano nikuwa matokeo ya watu wengine yamewekwa kapuni na kutoa yale wanayoyataka. Halafu utafiti halisi umepelekwa kwa kamati ya ufundi ya sisiem kuifanyia kazi kuokoa mambo.
Hapo zamani watawala (wafalme) walikuiwa na wapiga ramli wao wa kuwatabiria au kuwataadharisha kuhusu matukio yatakayowasibu (Julius Ceaser - "Beware the aides of March", etc.). REDET ndiyo wapiga ramli wa CCM/Kikwete. Oh, na Sheikh Yahya.REDET nao mara nyingine wananishangaza sana na hizi tafiti zao. Zinaleta tija gani?
Wanajidanganya..Hawatazifikia hizo asilimia lakini pia hivi asilimia 70 ni kishindo?REDET ni wale wale tu...Tusubiri Oktoba tuone.