Kikwete na kiu yake ya kukumbukwa kama Rais aliyetuletea maendeleo!

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,468
Reaction score
911,184



Daraja la Mkapa na bado yuko hai, na lipo Daraja la Kikwete........misifa hii haina tija hata chembe!





Jk na wapambe ndani ya ccm..............

Kiu ya JK kukumbukwa inazidi kushamiri na sasa anataka akumbukwe kuwa Raisi aliyetuletea maendeleo!

Tatizo liko wapi hapo?

Yapo maeneo mengi ambayo yanadhihirisha ya kuwa JK haelewi historia huwa inakuja kinyume chake:-

Hebu tuangalie maana ya maendeleo ni nini?

1) JK kama Raisi aliyemtangulia Bw. Mkapa wote wamefululiza kuhakikisha wanakumbukwa kwa kuitwa majina yao kupitia miundo mbinu kubwa kubwa......................JK alipoona daraja kubwa kule kusini Mkapa kalibatiza kwa jina lake basi naye akaliita daraja la Kigoma kwa jina lake!

Mkapa katoa mfano mbaya kwa JK na JK kwa vile ni "fokopi" akaona upuuzi ule nao wafaa kuigwa! Kosa moja haliwezi kuhalalishwa na kosa la pili.


Tatizo hapo ni kuwa miundo mbinu huchoka na baadaye kubomolewa na huo huwa mwisho wa utukufu wa ukoka ambao vinara hawa wamejipachika nao bila hata ya kutuuliza sisi waajiri wao!............

2) Tangia tupate uhuru tulitambua maendeleo ya kweli ni ya watu na wala siyo vitu kama miundo mbinu na hii miundo mbinu in walakini zifuatazo:

i) Inajengwa kwa bei za kutisha na wala ankara tajwa hazina uhusiano na bei za sokoni hivyo kuwa mzigo mkubwa kwa mwananchi. Badala ya nchi kufanya mambo mengi kwa "vijisenti" hivyo hivyo hujikuta tukifanya machache mno. Ufisadi ni sehemu kubwa inayosababisha hali hii...........

ii) Azma ya serikali kupitia "bomoa-bomoa" na tafsiri zake feki za sheria za ardhi zimefilisi raia wengi na kufanya miradi mingi hususani ya barabara kuwa mzigo mkubwa kwa jamii.

iii) "Bomoa bomoa" ikiambatana na sera ya ccm ya
"mpishe mwekezaji" imetuacha wakiwa na wanyonge ndani ya nchi. Jk kama angelikuwa makini katika kuenziwa na historia angelihakikisha sheria zinaundwa za kutulinda badala ya kutudhalilisha na fidia kiduchu kwa miliki ambazo tunaporwa......

iv) Karibu sehemu kubwa ya ujenzi wa miundombinu hapa nchini haujatumika kusaidia kupunguza tatizo la ajira hapa nchini na matokeo yake miundombinu lukuki inajengwa bila ya kusaidia kuendeleza wataalamu wetu kwa kuwapa changamoto.

Visingizio vya ya kuwa hatuna vifaa au uzoefu vinazidi kuthibitisha serikali ya JK haijali kabisa kuendeleza uwezo wetu wa kutatua matatizo yetu kupitia mikopo nafuu na kuzigawanya kazi kuwa ndogo ndogo na hivyo kutoa mwanya kwetu kuzifanya.

Pia serikali ya JK hudai kuwa kampuni zetu ziungane bila kutathmini kwa nini ujamaa na hasa vijiji vyake vilishindikana.....................na hivyo kutokuwa makini katika kuitumia historia yetu katika kujiletea maendeleo.................


3) Miundo mbinu nyingi hazidumu kutokana na usanifu na usimamizi bomu. Gharama za kurekebisha haya mapungufu zinatishia huduma nyingine za umma kwa sababu pesa nyingi hutumika kurekebisha mapungufu haya bila kuwepo kwa uwajibikaji kwa wakorofi wachache ambao hulitumbukiza taifa kwenye kiama hiki.

4) Huduma za umma katika kila sekta zimezorota mno na hata kuhatarisha maisha ya wananchi na huu siyo mkakati wa kujenga mazingira ya kukumbukwa vyema.

Soma makala hii kwa mfano wa ziada

www.jamiiforums.com/jf-doctor/394570-huduma-hospitali-za-umma-zinatisha-and-the-way-forward.html

5) Waswahili husema "Hujafa hujaumbika".......ndiyo ushauri wangu kwa JK kuwa akisha kufa ndipo jamii itamtendea haki lakini anapokuwa madarakani aache kujisifia na kufikiri anaweza kuiandika historia atakavyo bila ya kujua historia huandikwa na vizazi vijavyo ambavyo hata havitakuwa vikimfahamu yeye katika uhai wake................na kwa kuanzia angelikataza kiongozi yeyote wa umma aliyepo madarakani kutumia madaraka yake kujijengea umaarufu wa bei poa kama wa kuvikwa vilemba vya ukoka kupitia miundo mbinu ya nchi kama madaraja n.k

Na kila anayejikuza machoni pa mwanadamu Muumba humshusha chini na kuwa kichekesho kitupu machoni pa jamii ambayo mwathirika alinuia imtukuze......................ni kinyume chake huwa............jifunzeni haya........
 
I wishes were horses, everyone would ride one.
Tu mabingwa mno wa kupanga, lakini tunasahau kuwa ili unachpanga kionekane kuwa ni cha maana inabidi kitekelezwe. Lakini sisi tukishapanga, tunaangalia uzuri wa mipango yetu na kujiona tayari tumeshafanikiwa. Ndio maana mpaka leo nyimbo zetu ni hizo hizo lakini ukweli unabaki kuwa pale kuwa tumeshindwa, miaka 50 baada ya uhuru
- kuunganisha wilaya zote kwenye grid ya umeme ya taifa
- kuunganisha makao makuu ya wilaya kwa barabara zonazoipitika muda wote (si lazima ziwe za lami)
- kuhakikisha kuwa elimu inayotolewa inamwezesha mwananchi kuzalisha ajira na si kuwa mtafuta ajira
- kudhibiti matumizi ya rasilimali za taifa kwa manufaa ya wananchi wote kwa kuangalia na mgawanyo wake nk nk nk
Haya ni mambo machache kati ya yale makubwa ambayo tulitarajia kuwa taifa lenye umri wa miaka 50 na aina ya rasilimali ziomo ndani yake tusishindwe kuwa tumeyatekeleza. Lakini mpaka leo bado ni ndoto na viongozi wetu, badala ya kutusaidia kuzitekeleza ndoto hizo, wao wanatusaidia kuendelea kuziota
 

Mpita Njia tuna Raisi ambaye hata haoni soooooooooo kusubiri waajiri wake ambao ni sisi kumpima na kwa hiyo anajipima mwenyewe tena kwa mizania ambayo siyo aliyoombea ajira yake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…