Kikwete: Niliumia sana kundi la TMK kuvunjika, nilimuita Juma Nature Ikulu akakataa kusuluhishwa

Kikwete: Niliumia sana kundi la TMK kuvunjika, nilimuita Juma Nature Ikulu akakataa kusuluhishwa

britanicca

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Posts
16,295
Reaction score
33,994
Katika mazungumzo ya Kikwete na Mwanahabari maarufu alieleza jinsi alivyopata ushindi mwaka 2005, akaeleza mchango wa wasanii katika siasa za Tanzania.

Anaeleza kwamba kwa kiasi kikubwa alisaidiwa na kundi la Wanaume TMK kuteka hisia za vijana kwa kipindi hicho.

Nililipenda kundi lile lililoongozwa na Juma Kassim, ambaye watu wanamjua kama Juma Nature, kwa kifupi alifuatwa kutusaidia kwenye kampeni, uzuri hawakuwa na mlolongo sana ni kupangiwa ratiba wakakubaliana na sisi.

Nilisikitika sana mwaka 2006 Kusikia kundi lile limesambaratika.

Niliwaita Ikulu kwa ajili ya usuluhishi lakini Bwana Juma hakutokea, nilikutana na Wengine mfano Chege na Somebody Temba, walikuja mara kadhaa.

Kilichoharibu zaidi makampuni yakatumia ugomvi wao kutengeneza hela, nao wakirubunika kwamba matamasha yale yatawapa hela kwa muda mrefu, kumbe walihitajiana sana kusonga mbele,

Alisema Kikwete alipokuwa na mazungumzo na gazeti la The Citizen.

Pitia pia

 
Sio siri jamani jk ukimsikiliza kwa makini huyu mzee ana maono mazuli anaona mbali mnoo

Maneno ya huyu mzeee kwa watu wenye akili kuna vitu tumejufunza kuhusu maisha ya kwamba "majuto ni mjukuuu" huyu juma nature kama angetulia Leo hiii angekuwa mbalii mnooo britanicca,
 
Back
Top Bottom