Masako wa ITV-Asilimia zaidi ya 80 ya watanzania wanategemea kilimo, miaka mitano iliyopita, bado wana matatizo ya masoko na wanauza kwa bei anayotaka mnunuzi. Umefanya nini kuwasaidia, na miaka mingine mitano umepanga kuwafanyia nini?
JK-Tumepanua lilomo cha umwagiliaji, katika ASDP asilimia 75 ya pesa ni za umwagiliaji kuongeza matumizi ya mbegu bora, mbolea, madawa, maofisa kilimo wawafundishe wakulima kanuni za kilimo bora, kuboresha masoko na bei, kuboresha barabara, kuanza safari polepole lkn kwa uhakika kutoka kutegemea jembe la mkono tutumie matrekta.