kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Siku moja nilisafiri kutoka mkoani kuja Dar es Salaam kwa basi, siti niliyokaa kulikuwa na mama mmoja tulikaa siti moja, njia tulikuwa tunapiga stori kwa furaha. Lakini tulipokaribia Mbezi ya Kimara yule mama akakurupuka na kutafuta lile vazi la kiislamu la kufunika uso na macho yote kwenye begi lake. Nilimshangaa kwanini alikuwa kichwa wazi safari nzima na sasa ndo anafunga qarb machoni. nilipomuuliza kulikoni akasema mume wake ndiye anamlazimisha kuvaa vazi hili, hivyo itakuwa ugonvi mkubwa kama atamkuta mumewe Ubungo stendi kumlaki. Mama alikuwa akiongea kwa uchungu juu ya vazi hili. Na si huyo tu hata rafiki yangu kwa sababu ya wivu amemlazimisha mkewe afunike uso na macho akitoka nje.
Ombi kwa Rais na wabunge, inaonekana kuwa wako wanawake wengi na watoto wa kike wanaolazimishwa kujigubika gubigubi iwe kunajoto, jua, mawingu, mvua n.k bila hiyari yao kwa amri za waume/baba zao, jee wanawake hawa utawasaidiaje? huoni raia wako wako utumwani mwa matalibani? Bora uwepo mpango wa kuwabaini wanawake waliolazimishwa na waliovaa kwa hiyari yao.