Elections 2010 Kikwete sasa Mzigo CCM

Nyambala

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2007
Posts
4,465
Reaction score
1,171
Katika hali ya kustaajabisha ndani ya campaign trail inaripotiwa kwamba mgombea wa uraisi kwa tketi ya CCM hauziki. Hili linasemwa chini chini na wenyeviti wa CCM wa wilaya kadhaa. Kutokuuzika kwa mgombea huyo kunahatarisha hata baadhi ya wagombea ubunge na madiwani wa CCM.

Sababu kuu za kuporomoka kwa nyota (kama yeye mwenyewe anavyopenda kuiita) ya mgombea uraisi wa CCM ni kama zifuatazo.

1. Mgombea na CCM hawakujiandaa kabisa kupata resistance wanayoiona.

2. Loyalty kwa chama imepungua mno au haipo kabisa kutokana na CCM kuweka bei ya karibu kila kitu kuanzia support, attendance ya mikutano na hata kura zenyewe. Sababu nyingine ni majority ya voters wa sasa hivi wengi ni born in the eightees and ninetees hivyo impact ya CCM kama influence haipo.

3. Pamoja na kusifika kote kwa strategy na organaizesheni CCM this time imekabidhi zigo zima la strategy kwa mgombea mwenyewe na familia yake.

4. Same old rhetoric kuendelea kutumika kwa kudhania watanzania hawa ni wale wale wa yes sir.

5. Sababu nyingine ni over-confidence aliyokuwa nayo JK kabla ya kampeni kuanza, hasa ukizingatia ushabiki na support fake (yes it was bought) wakati utaratibu wa kumpitisha ndani ya chama chake ulipokuwa ukiendelea. Alisahau kabisa kwamba wale walikuwa ni mainly wanaCCM na sio watanzania wote.

6. Uchakachuaji wa kura za maoni of which hakuonyesha leadership kufikia maamuzi ya mwisho.

7. Kuwazuga watanzania kwamba yeye ni mpambanaji wa ufisadi wakati huo huo akiwasafisha watuhumiwa ufisadi na akikampeni kifisadi. Funny enough thse day kila anapoenda watu wenye questionable credibility ndiyo wanakuwa mstari wa mbele kuwa naye karibu.

8. JK anadhani yeye ndiye CCM na CCM ndiyo yeye na yeye ndiyo serikali, which is absolutely very wrong.

9. Makamba, Kinana, na baadhi ya mafisadi kudhania kwamba they can do it alone..... Waliwakejeli vigogo wa zamani wa chama hicho na hawakutaka kuwahusisha kabisa na mwenendo wa kampeni utakavyokua.

10. Sababu kuu na muhiimu kuliko zote WATANZANIA WAMEICHOKA CCM na ahadi zake hewa, wanamwona kikwete kama nabii wa uongo, tapeli na asiye na chembe ya ujasiri wa kuwaafikisha kule wanakokutaka.
 
Wa kina TINGA TINGA!!!

Wamemtosa mzee wa watu, sasa hali mbaya!! Ulimi nje nje!!
Kazi wanayo, ila ushauri wa bure kwa CHADEMA, never underestimate the capacity of this monster!!! It can do anything with in its power on seeking re-election.

:hand:
 

hayo ndo nadhani makubwa saana yanayomletea natatizo mpaka saizi au ndo kelele za mlango hazimzuii mwenye njyumba kupata usingizi?????
 
Kwa kampeni za CCM kuachiwa familia ya JK naona apo kwa kweli wamemsusia ilo zigo.
Madakatari wake wawe wanacheki BP daily as anything can happen
 
Inaripotiwa wapi na nani? Au ni haya mambo tunaona kwenye TV akiwa mjini. Kumbuka vijijini wapiga kura wengi bado wana kasumba ya CCM na wanatishwa na kutishika. Let us avoid making sweeping statements. Tutake tusitake bado CCM ni monster na aitashindwa kwa wishful thinking.
 
Kikwete ni Mbishi sana.....huwezi kufanya naye kazi ...Mwache achume matunda yake...
 

Well said.
 

Nyambala, you are a very good analysi. Cheers
 

Mkuu hizi nni habari kutoka huko huko unakoita kijijini ni habari za kuaminika as reported by me from a highly trusted and reliable source, Nimepewa mifano Majimbo yafuatayo kutoka mikoa ya nyanda za juu kusini yameponyoka na nguvu kubwa mno inahitajika kuyarudisha CCM

1. Mbarali
2. Mbeya Mjini
3. Mbozi mashariki
4. Mbozi Magharibi
5. Iringa mjini
6. Njombe kusini
7. Njombe kaskazini
8.Sumbaawanga mjini
9.Nkasi kusini

Habari ndiyo hiyo!

Just stay tuned!
 
Watu wanaomfahamu hata alipokuwa jeshini tena alikuwa analala naye hanga moja anasema JK ni mtu mwenye chuki binafsi, mpenda wanawake na mdini kupindukia. Nadhani chuki binafsi ndo imewaweka wazee na wenye busara kama Salim Ahmed Salim pembeni. Hawataki kujihusisha hata kidogo.
 
Kikwete ni Mbishi sana.....huwezi kufanya naye kazi ...Mwache achume matunda yake...
Sasa kwa kutambua hilo natumaini kura yako utaielekeza kwa Dr wa ukweli na sio Dr wakupewa kama njungu kama wa wakina Dr Cheni, Dr L Abdalah, Dr Manyaunyau nk
 

NYambala, unweza mtumia hii kitu yule mwandishi wa habari wa Kikwete Maggid Mjengwa?
 

sababu kubwa inayowafanya wazee wa cccm kama vile mkapa, mwinyi, malecela, warioba n.k kujiweka pembeni na kampeni za jk za 2010, ni woga wa kufikishwa katika mahakama ya kimataifa ya makosa dhidi ya ubinadamu endapo yatatokea mauaji ya aina yoyote hapa nchini baada ya matokeo ya uchunguzi kutangazwa.

mahakama kama hiyo ilifunguliwa kushughulikia viongozi wa nchi ya rwanda waliohusika na kupanga na kuchochea mauaji ya halaiki na ina makao makuu yake mjini arusha,tanzania. Mahakama hiyo hivi sasa imeshatoa hati ya kukamatwa kwa jenerali omar el-bashir wa nchi ya sudan

aidha mahakama hiyo ipo mbioni kufungua shughuli zake nchini kenya kuchunguza na hatimaye kuwafikisha mahakamani wote waliohusika kwa namna moja au nyingine na kuvuruga uchaguzi mkuu uliopita nchini kenya na kuchochea mauaji ya kinyama.

wazee wa ccm wanazo taarifa ya mipngo ya jk kutumia jeshi ndio maanaa hawataki kuhusika na kampeni wasije kusekwa ndani, endapo jk ataamua kutumia jeshi kupora ushindi wa wapinzani.
 

Ukweli ni kwamba viongozi wakuu wa zamani walimtaka kikwete amuondoe Makamba kwenye nafasi ya katibu mkuu CCM ili waweze kushirikiana nae katika kampeni lakini yeye akawapuuza. walimwambia makamba hana credibility ya kuwa msemaji wa chama hivyo wakishirikiana nae wakati makamba yupo nao wataonekana wapuuzi kama makamba

Angalia Kikwete ameenda Hanang na Sumaye siku moja kabla akatoka Hanang kuja DSM. Vivyo hivyo kwa Mkapa
 

Inaelekea hata pesa ya kampeni ishaanza kupungua!!
 
Hili nalo neno sana, JK hana sera, Zile kesi mahakamani ni usanii mtupu hili apate ujiko toka nje na hata ndani, Masikini mseminari waliona awe chambo pale BOT, Kwakuwa yeye hakuwa na GODFATHER ndiyo maana hakufa kama Balali.
 

I see!! well said. I have never heard any concrete point from this man, Ever since I knew him.
 
Hapo umenena:-

10. Sababu kuu na muhiimu kuliko zote WATANZANIA WAMEICHOKA CCM na ahadi zake hewa, wanamwona kikwete kama nabii wa uongo, tapeli na asiye na chembe ya ujasiri wa kuwaafikisha kule wanakokutaka.

Ukichanganya na hii kutoka kwa QUALITY basi JK ukweli wake upo mezani na sote sasa tumemfahamu:-



Lenye mwanzo halikosi mwishooooooooooooooooo........................na mbio za sakafuni huishia ukingoni...........................
 
Halafu gonjwa ndiyo linazidi kuchanganya, loo ,masikini kifaulongo JK !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…