Kikwete sawa UDOM, na Vyuo Vikuu vingine?

Kikwete sawa UDOM, na Vyuo Vikuu vingine?

Iga

Senior Member
Joined
Dec 17, 2007
Posts
112
Reaction score
6
MAPENZI aliyeonesha Mheshimiwa kwa Chuo Kikuu Dodoma laiti pia yangelipewa angalau nusu vyuo vingine hakika malalamiko mbalimbali ya wanavyuo yangelipungua kwa kiasi kikubwa.

Vyuo vingi hapa nchini vina uwezo wa kuingiza mapato makubwa na bado wanafunzi wakaweza kusomeshwa kwa wingi na kwa kiwango cha juu kuliko ilivyo sasa.

Kinachotakiwa ni kuangalia hali halisi ya maisha na uwezeshwaji wa vyuo hivyo kujipanua kwa kupewa fedha ya mbegu kwa mambo mbalimbali ambayo baadaye yatajitegemea na kuingizia vyuo hivyo pato la haja,

Kwa mfano, ndio tuna Chuo Kikuu tena kizuri sana cha Dodoma lakini tukumbuke pia kwamba tuna Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ( Open University of Tanzania) ambacho wananchi wengi hawakijui hadi wa leo ingawa kimeanza takriban miaka 20 iliyopita.

OPEN UNIVERSITY OF TANZANIA kama kikiwezeshwa kina uwezo wa kuwa na Chuo Kikuu katika kila mkoa hapa Tanzania. Tuseme kila mkoa katika University college yake chini ya OUT kikiwa kinapokea wanafunzi elfu mbili tu basi Chuo Kikuu Huria kina uwezo wa kuwa na wanafunzi 52,000 fumba na kufumbua nchi nzima.

Kinachohitajika ni kwa serikali kuwezesha chuo hicho kuboresha majengo yake inayomiliki hivi sasa na pia kununua yale inayokodisha. Kisha kiwezeshe kuwa na masomo yote inayosomesha kwenye mtandao yatakayoandikwa na walimu wake wenyewe. Walimu hao lazima walipwe kwa kazi hii ya kuandaa vitabu maana ni nje ya kazi za kawaida.
 
Back
Top Bottom