S. S. Phares
JF-Expert Member
- Nov 27, 2006
- 2,138
- 85
Tatizo la hali ya hatari na hizo unazosema imergence laws, zinaweza kukosa macho na kuwakumba hata wasiohusika (inaweza kutumika kulipa visasi). Unaweza kushangaa hata wewe, JF ndani kwani inategemea utashi wa wanaoendesha operation. Ni rahisi kutamka ila shughuli yake ni hatari.
Mkuu Mwanakijiji heshma mbeleasithubutu kutangaza hali ya hatari... ni wazo baya na wazo la hatari kufanya hivyo.
he means STATE OF EMERGENGY? emergency - an unexpected and sudden event that must be dealt with urgently. kwahiyo hili suala la ufisadi ni sudden event ambayo inatakiwa ishughulikiwe kwa uharaka hili kuliondosha? msaada wataalam.
Hali ya hatari, mara nyingi, huendana na mambo yafuatayo:-
a. Utawala wa amri (ki-imla)usiozingatia au kuheshimu sheria;
b. Kufishwa kwa uhuru wa vyombo vya habari;
c. Kuundwa kwa tribunals kuchukua mahali pa mahakama;
d. Uongozi wa nchi kutegemea mawazo na utashi wa viongozi waliopo madarakani bila kuwa challenged na chombo chochote;
e. Kupunguzwa kwa Uhuru wa kutembea, kuzungumza na hata kuwaza na kupasha habari;
f. Polisi na majeshi kuwa na nguvu zisizo kifani katika kukamata raia na kuwadhibiti.
Kutokana na hayo, hili la hali ya hatari mmmh! Kiula aje na lingine. By the way, situation kama hii ingekuwepo wakati wa kesi yake angechukua mvua si chini ya 30.