Kikwete: Tutawajibu wanaotusema!

Mambo ya Politiki za bongo ni uvundo mtupu...Kwani huyo JK hataki watu wamwambie kuwa anatokota wakati mchezo ndio unaanza?? Si mlikuwa mnataka Raisi mwenye sura nzuri ndio huyo sasa....

Lakini jamani si munajua tena matatizo ya uzuri?waangalieni ma model wetu wanavyo ishia nasisi hatukuchagua kiongozi tulichagua model hayo ndio matokeo yetu
Lakini kijana ndio mtaji analipa kwa mujibu wa mzee jangala [makamba] sasa tunatakanini tena?
 
Watanzania hebu tuwe wakweli na kumuogopa Mwenyezi Mungu. Kongamano la Mwalimu Nyerere halikuwa na lolote baya zaidi ya kuelezea hali halisi ya nchi yetu ilivyo hivi sasa kutokana na mengi yanayosemwa na wananchi mitaani. Tukumbuke kwamba viongozi wetu wanawajibika kwa wananchi waliowapa dhamana hatukuwaweka pale ili wawe wanafanya wanavyotaka wao bila kujali hisia, matatizo ya wananchi na maslahi ya taifa kwa ujumla.
 
Mwisho tunakupenda sana raisi wetu ila ukiendelewa kuwalea marafiki zako basi tena SISI WAZANAKI KUNA MSEMO TUNAITA " MALI GANYANJAA...

Naomba kukusahihisha kwa usemi huu: Kwanza nina hakika wewe siyo mzanaki kwa vile neno uliloandika halimo katika lugha ya Kizanaki. Na hakika hiyo naipata kutokana na watu wengi kufanya makosa kwa kutumia neno hilo ambalo alitamka hayati Mwalimu Nyerere wakati akielezea mchukua rushwa na mtoa rushwa kuwa 'WOTE NI MANJI GA NYANCHA'.

Msemo huu mwalimu aliutoa kumaanisha kuwa wote mtoaji na mpokeaji ni Moto. NYANCHA ni jina la Kijiji Musoma wilayani Bunda ambalo lilikuwa na Chemchem inayotoa maji ya Moto na watu walipenda sana kwenda pale kuoga. Hivyo aliposema kuwa WOTE ni Maji (MANJI) GA kiunganishi cha (ya) NYANCHA ambayo ni ya moto.
 
wakati nyie mnaonekana kukunja nyuso kwa kile alichokitamka mzee wa chalinze kuwajibu wabaya wake, wapo wanaofurahia ujasiri wake katika kuwajibu hao wanaomwandama (kama wapo na kama kweli wana chuki binafsi) anyway hilo nitunda la makada na ambalo si ajabu litarudi tena mwakani. itakuwa ni ajabu kumshangaa sofia simba wakati wanaotakiwa kukemea ndo majibu yao hayo. tumekwishaaaaaaaaa.
 

Mimi nasubiri majibu ya Rais kuhusu tuhuma hizi ndipo nitajadili.Na ajibu kweli asiishie kusema tu kwamba atajibu mapigo
 
Kikwete sasa ndio ameharibu kabisa, hayupo kabisa kwenye hadhi yaakina jaji warioba, mheshima butiku na salim ahmed salim pamoja ya kuwa yeye ni raisi wa nchi. Si busara hata kidogo raisi wa nchi akasimama na kujibu shutuma zinazomhusu kabisa kihuni namna ile na ukizingatia kuwa zimetolewa na watu wenye heshima na hadhi kubwa kiasi kile. Kwa heri mzee wa kutabasamu.....umejichimbia kaburi lako mwenyewe
 

Mtashauri weeeee lakini kumbukeni kuwa Kenge daima haachi mila zake mpaka damu itoke masikioni
 

Asante kwa tafsiri nzuri, kwa hiyo na Tarime ni "Manji ga Nyancha?
 

Siyo wanyawezi tu wanye mawazo ya kwamba bila CCM hakuna maisha, bali ni watanzania wengi na hasa watu walioko kwenye vyombo vya dola kama polisi, UWT na hata tume ya uchaguzi yenyewe, kwa hiyo mabadiliko ya mawazo yanahitajika kwa kundi kubwa
 
Na Sadick Mtulya





Kikwete anatarajia kuongoza msafara wa watu takribani 60 atakapokwenda Copenhagen kuhudhuria mkutano wa Mabadiliko ya Tabia Nchi ambao utahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa.

Jamani , 60 people are going to Copenhagen.I would like to know the credentials of those people and who will pick up their tabs (cover their expenses). Lasty, what are going to benefit as a country from that meeting.
 
Asante kwa tafsiri nzuri, kwa hiyo na Tarime ni "Manji ga Nyancha?

Tutahamisha mada nikianza kujibu na hayo unayouliza ya Tarime, niliamua kumfahamisha hilo huyo kutokana na ukweli kuwa watu wengi wamekuwa wakilitumia neno hilo isivyo sahihi. Nakumbuka siku moja neno hilo pia limewahi kutumiwa na Mkuu wa mkoa katika moja ya hotuba zake akatamka MADI GANCHA akimaanisha kuwa serikali itawasaka wanaohusika na mauajia ya Albino na kuonya kuwa wanaoua na Mganga eote wakikamatwa ni MADI GANCHA. Sasa wanalipotosha.

Ukweli unabaki kuwa kama hayo pia ndiyo majibu ya JK, ambayo hayatofautiani na yale ya Makamba, Sophia Simba basi wote ni MANJI GA NYANCHA. Wako kundi moja la Maji Moto kutoka Nyancha.
 
Tanzaniaaa,Tanzaniaaaaaaaaa, nakupenda kwa moyo wote....kazi ipo
Hapo nyuma kikwete alipoingia madarakani niliwahi toa mfano wa utawala wa ukraine kwa Viktor YUSHCHENKO,aliingizwa madarakani kwa mbwembwe nyingi aliposhindwa kudeliver (kutoa maisha bora ).2007 akawa ni moja ya watu wanaochukiwa huko Ukraine.nikasema kwa ahadi ya maisha bora ya CCM lazima yatamkuta tu muungwana,nadhani tunaanza kuelekea huko taratiiibuuuuuuuuuuuuu
 
hahaha huwa nikiwa nataka kucheka najaribu kuingia jf maana watu humu wako na character za aina mbali mbali kutokana na majibu yao mweeh!.....it is very restaurante!....LOL!




Duh!!! stimu unachukulia kwa jirani................
 

Taja majina ya mashemeji wa Nyerere aliowateua, au futa usemi wako?
 


Maneno ya Nyerere yanakaribia, naona mgawanyiko huu utaleta CCM Asili na CCM kandambili,ndani ya chama na baada ya hapo kutakuwa na hesabu hii...15% (CCM asili) + 70 (bendera fuata upepo?) = 85% - 30% (mafisadi kununua kura) = 55%...hapo naona CCM kandambili hana bao na tutakuwa tumepata chama ambacho Nyerere alikwisha kitabiria kuwa ni wanachama wa CCM pekee wenye ubavu wa kuing'oa CCM, hebu fikiria leo hii, Butiku, Warioba, Mzee Mangula, Tingatinga, Salim A Salim, changanya na wapiganaji walio mstari wa mbele wote waanzishe timbwilitimbwili la ndani ya chama na kufanikisha kuunda "CCM asilia" rasmi (sasa sio rasmi bali ni makundi tu)
 
Naona aibu kusikia majibu rahisi ya maswali magumu toka kwa mkuu wa kaya, am not proud of him at all for his simplicity. I wished he stepped down before 2010...
 
Mchangiaji mmoja kwenye Kongamano alisema anayo machache ya kusema kama ifuatavyo:
Kwanza wahenga wanasema “Kiongozi ni Jalala.” Maana yake ni kuwa lazima awe tayari kuwasikiliza wale anaowaongoza. Ayasikilize yote yale yanayompendeza na anayotaka kuyasikia lakini pia yale ambayo hayapendezi asingependa kuyasikia: ni lazima ayasikilize yote. Jalala hupokea majivu ya moto na yaliyo baridi. Kwa hiyo kiongozi lazima awe mvumilivu. Kiongozi awe mtu wa subira.
Kiongozi hana budi kuwa muwazi na mwenye msimamo na mwenye uamuzi ulio wazi. Kiongozi lasima awe na uwezo na sio uwezo tu bali afanye uamuzi na hasa juu ya mambo ya msingi. Kutojulikana msimamo wa kiongozi au kubabaika katika msimamo kunakwaza na kuwababaisha wale anaowaongoza. Msimamo wa kiongozi lazima ujulikane ili raia au anaowaongoza wafanye uamuzi wa kumuunga mkono au vinginevyo. Na kwa kufanya hivyo Kiongozi atajua mawazo ya wale anaowaongoza kama wanamuunga mkono au vinginevyo.

Kiongozi lazima asiwe na makundi: kundi lake na kundi lao. Achukie makundi yenye kuhasimiana katika jamii.

Kiongozi lazima atetee haki ya watu wote na awe kimbilio la wanyonge. Wakati wenye nguvu wanaweza kujitetea na kusimamia mambo yao wenyewe, kiongozi lazima awe mtetezi na kimbilio la wanyonge. Kama kiongozi akijitambulisha na wenye nguvu wanyonge watatetewa na nani?

Kiongozi lazima awe msimamizi wa ugawaji wa rasilimali za nchi kwa haki na usawa bila upendeleo.
Kiongozi awe mfano kwa kauli na vitendo vyake. Kiongozi ajue amevaa koti jekundu kila anapokwenda na kila analolotenda linaonekana kwa watu.
Kazi moja muhimu ya kiongozi ni kulinda uhai na maslahi ya kila raia na jamii kwa jumla. Katika kutetea haki na uhai wa kila raia viongozi wafanye jitihada kubwa ili waweze kumwambia Mwenyezi Mungu kuwa walifanya jitihada ya kuwalinda wale wanaowaongoza na waweze kusema “katika wale ulionipa sikumpoteza hata mmoja.” Iwe ni kero, iwakere viongozi kuona raia wao wanapoteza maisha iwe kwa ajali ya magari, ushirikina na tamaa ya mali au ujambazi.......n.k.
 


Bora angemchukua na mama wa mipasho Sofia Simba nae akapime akili
 
amesema atapumzika mwanzoni mwa mwaka,
nadhani atarudi tena iringa kwa wakwe zake pale kwa asas maana ameoa pale majuzi.

huku iringa wanamwita shemeji wakwe wapo .

halafu naomba kusaidiwa hivi huyu jamaa huwa anawaona vipi hawa mabinti au kuna mtu anapiga pande? maana toto la kiarabu la mzee asas si chezo. aklidanganya taifa kuwa yuko mapumzikoni ruaha national park kumbe yuko ukweni!!!

MI NAWAMBIA HUYU TUTAMTUPIA MAWE AKIMALIZA KIPINDI CHAKE.
 
Siamini kama Rais wa nchi anaweza kujibu hivyo anaonewa wivu???? ni lini JK ataamka aongoze nchi badala ya kuendekeza U-Vasco Da Gama???? anaona sifa eti nani ataenda kwenye mikutano,sasa nani anamfanyia kazi zake pale magogoni???? kama wanaweza iweje kwenye ruti ndo wasiweze!!!!!!
Sio kila ishu unaweka utani,waswahili tuko siriazi na umaskini...... tafadhali mkuu!!!
Subira yavuta heri hii inavuta shari kaa mkao wa kula...
Endelea kuwalinda wote wanaofanya maisha yetu yawe miserable hasa hao wahindi eti wa-tz.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…